Heshima
ya mshambuliaji, Mbwana Samatta inazidi kupanda katika kikosi chake cha
KRC Genk ya Ubelgiji na sasa achukuliwa kama moja ya wachezaji muhimu
zaidi klabu hapo.
Hiyo inatokana na Samatta kuwa miongoni mwa wafungaji mahiri kwenye ligi ya Ubelgiji, Pro League, na tayari ana mabao manne.
Wakati
anasajiliwa na Genk akitokea TP Mazembe ya DR Congo, haikuwa rahisi
kuona Samatta akiwekwa kwenye matangazo muhimu ya Genk (Poster).
Kutumika
kwenye matangazo ni sehemu ya kuonesha una mvuto au unakubalika. Jambo
ambalo ni bora kwa Samatta na anachotakiwa ni kuongeza tu juhudi.
Ikumbukwe
kwamba Genk alifuzu kucheza hatua ya makundi ya Uefa Europa League
msimu huu na walipangwa kundi F na timu kubwa kama Athletic Club ya
Hispania (kama inavyoonekana chini na ratiba ya mechi zenyewe).
Tayari Genk wameanza kuzitangaza mechi zao kwa kutumia wachezaji wao muhimu akiwemo Mbwana Samatta (Tazama picha juu).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni