TIMU ya Simba imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Maafande wa Ruvu Shooting katika muendelezo wa ligi kuu ya Vodacom mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Iliwachukua dakika saba Ruvu kupata bao lililowekwa kimiani na Abraham Mussa kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango Vicent Angban baada ya mabeki wa Wekundu hao kuzembea kuondoa hatari.
Dakika tatu baadae Ibrahim Ajib aliisawazishia Simba kufuatia pasi safi iliyopigwa na winga Shiza Kichuya upande wa kushoto wa uwanja baada ya Maafande hao kushindwa kujipanga vizuri.
Mshambuliaji Laudit Mavugo alikosa nafasi za wazi dakika ya 19 na 23 baada ya Ajib kufanya kazi ya ziada kuichambua safu ya ulinzi lakini Mrundi huyo alikosa umakini.
Mavugo aliipatia Simba bao la pili dakika ya 48 baada ya kupokea pasi nzuri ya Ajib ambaye alikuwa mwiba mchungu kwa mabeki wa Ruvu.
Mwamuzi Ngole Mwangole kutoka mkoani Mbeya alimuonesha kadi nyekundu kiungo Jabir Aziz baada ya kumfanyia madhambi Muzamir Yassin.
Simba iliwatoa Mavugo, Saidi Ndemla na Kichuya nafasi zao zikachuliwa na Fredrick Blagnon, Muzamir pamoja na Jamal Mnyate. Kwa upande wa Ruvu waliwapumzisha Frank Msese, Abraham Mussa na Claide Wigenge na kuwaingiza Baraka Mtui,Issa Kanduru na Renatus Kisase.
Huko mkoani Mtwara, Yanga imeshindwa kufurukuta baada ya kutoka suluhu na Ndanda katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Nangwanda Sijaona.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Hanse Mabena wa Tanga aliyesaidiwa na Nicholas Makaranga wa Morogoro na Hajji Mwalukuta wa Tanga, Ndanda itabidi wajilaumu kwa kushindwa kupata bao, licha ya kuwazidi kimchezo Yanga.
Ndanda waliutumia vizuri Uwanja wa nyumbani kwa kutawala tu mchezo, lakini wakashindwa kumfunga kipa mzoefu wa mabingwa watetezi, Ally Mustafa ‘Barthez’.
Sifa zaidi zimuendee beki mpya chipukizi, Andrew Vincent ‘Dante’ aliyeua mashambulizi mengi ya hatari ya Ndanda pamoja na kuokoa mpira mmoja uliokuwa unaelekea nyavuni kufuatia shuti la Omary Mponda.
Kiungo mpya mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa alipoteza nafasi nzuri ya kufunga dakika ya 25 baada ya kupewa pasi nzuri na mshambuliaji mwenzake wa zamani wa FC Platinum ya Zimbabwe, Donald Ngoma.
Mzimbabwe Ngoma na winga wa Taifa Stars, Simon Msuva wote baadaye wakapoteza nafasi nzuri za kufunga.
Yanga kidogo ilianza kucheza vizuri kwa mwelekeo wa kutafuta bao dakika 20 za mwisho, wachezaji wake wakigongena vizuri pasi, lakini safu ya ulinzi ya Ndanda iliyoongozwa na Salvatory Ntebe ilisimama imara kutimua mipango yote.
Yanga ilipoteza nafasi nyingine nzuri ya kupata bao dakika ya 90 na ushei baada ya kupata mpira wa adhabu wa kupiga ndani ya boksi, kufuatia kipa wa Ndanda Jeremiah Kisubi kudaka mpira, kudunda na kutembea nao.
Wachezaji wa Yanga walilaumiana wenyewe kwa wenyewe baada ya mchezo ambao walikuwa wana matumaini makubwa ya ushindi.
Yanga inakamilisha michezo miwili ya Ligi Kuu, ikitimiza pointi nne, baada ya kushinda 3-0 mechi ya kwanza dhidi ya African Lyon, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wiki iliyopita. Kikosi cha kilikuwa Ndanda FC; Jeremiah Kisubi, Bakari Mtama, Paul Ngalema, Hemed khoja, Salvatiry Ntebe, Ibrahim Isihaka, Salum Minely/Nassor Kapama dk66, Salum Telela, Omary Mponda, Shijja Mkinna na Kiggy Makassy.
Yanga SC; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Andrew Vincent ‘Dante’, Thabani Kamusoko, Simon Msuva, Deus Kaseke/Juma Mahadhi dk58, Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Obrey Chirwa.
Kule Mbeya,Azam leo wameendeleza wimbi la ushindi baada ya kuibuka na ushindi wa bao
1-0 mbele ya Tanzania Prisons, mchezo uliofanyika katika Uwanja wa
Sokoine jijini Mbeya.
Katika
mchezo huo ambao ulikuwa mgumu kwa pande zote mbili kutokana na
kushambuliana kwa zamu, Azam walianza kulifikia lango la timu ya Prisons
mnamo dakika ya nne tu lakini kichwa cha Shomari Kapombe lakini kipa wa
Prisons aliokoa hatari hiyo.
Timu zote ziliendelea kushambuliana kwa zamu mpaka kipindi cha kwanza kinaisha, hakuna timu iliyopata goli.
Kipindi
cha pili kilianza kwa kasi ileile kwa timu zote kushambuliana kwa zamu,
lakini walikuwa ni Azam ambao walipata goli dakika ya 59 baada ya
kiungo wa timu hiyo Muivory Coast Kipre Bolou kupiga shuti kali
lililogonga mwamba akiwa ndani ya eneo la hatari na kutinga wavuni.
Baada
ya goli hilo Prisons walionekana kutulia na kushambulia kwa malengo ya
kusawazisha lakini hata hivyo ukuta imara wa Azam uliokuwa ukiongozwa na
Amoah pamoja na Mwantika uliondoa hatari zote na kufanya matokeo kubaki
1-0.
Kwa
matokeo hayo, Azam wanakuwa kileleni wakiwa na alama 7 baada ya kucheza
michezo mitatu sambamba na Simba lakini wakiwa na wastani mzuri wa
magoli ya kufunga na kufungwa.
2016-09-10
16:00 | MWADUI FC | Vs | STAND UNITED |
16:00 | MBEYA CITY | Vs | Azam FC |
16:00 | African Lyon | Vs | MBAO FC |
16:00 | NDANDA FC | Vs | KAGERA SUGAR |
16:00 | YANGA | Vs | MAJIMAJI |
16:00 | RUVU SHOOTING | Vs | JKT RUVU |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni