TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI;
MUHTASARI WA MKATABA.
1. Bodi
ya Wadhamini wa Young Africans Sports Club, (ambayo hapa inajulikana
kama Mmiliki”) imeingia tarehe 3 September, 2016 Mkataba wa kukodishwa
na kampuni ijulikanayo Yanga Yetu Limited (inayojulikana hapa kama
“Mkodishwaji” kwa muhtasari wa maazimio yaliyoafikiwa katika Mkutano
Mkuu wa Young Africans Sports Club uliofanyika tarehe 6 Agosti, 2016
ulitambua kuwa Young Africans Sports Club (anayejulikana hapa kama
“YANGA”):
1.1 KWA
KUWA, Timu ya Soka ya Mmiliki ni kongwe na yenye mafanikio kuliko timu
ya soka nyingine zilizoko katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yenye
thamani kubwa kiutamaduni na kwa urithi wa Taifa, licha ya jitihada zake
zote, inakabiliwa na changamoto za kifedha katika kuiendesha timu yake
ya mpira wa miguu, kwa kuwa na usajili mdogo wa uanachama, ukosefu wa
mapato, ya ada za Wanachama, mifumo isiyo na ufanisi ya kiuendeshaji,
kushindwa kujipatia kipato cha kibiashara kutoka katika hati miliki na
nembo za kibiashara za Timu ya Soka ya YANGA kutoweza kujiendesha
kibiashara na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Tanzania (TFF)- ambalo kwa
mfululizo linasababisha YANGA kuiendesha Klabu yake kwa hasara na kuwa
tegemezi kutoka kwa michango ya wahisani na kwa mikopo na kukabili
changamoto hizi; na Mkutano wa Wanachama wa YANGA tarehe 6 Agosti 2016
uliazimia kugeuza hali hii kwa kukodisha Timu ya Soka ya YANGA ambayo
ilikuwa inajiendesha kwa hasara na mapato madogo kupitia nembo yake na
hakimiliki yake (jina na nembo) kwa muda wa Miaka (10), ili kuikinga
Klabu kutoendelea kujiendesha kihasara katika kipindi cha Miaka (10) ya
ukodishwaji, ijipange kiuwezo ili Timu ya Soka ya Mmiliki na hakimiliki
za jina lake na nembo zitakapo rejeshwa baada ya kukodishwa kwa kipindi
cha Miaka (10), YANGA itakuwa inaweza kujiendesha yenyewe na iwe na
uwezo wa kifedha na iweze kushindana kikamilifu katika shughuli za mpira
wa miguu.
2. Yanga
Yetu Limited (inayojulikana hapa kama “Mkodishwaji”) ni Kampuni
iliyoundwa ili iweze kuingia katika Mkataba na YANGA ili iweze kutimiza
malengo ya Klabu kama yalivyo azimiwa katika Mkutano wa Wanachama wa
YANGA uliofanyika tarehe 6 Agosti, 2016.
3. Baraza
la Wadhamini wa Young Africans Sports Club baada ya mazungumzo na
Mkodishwaji linapenda kuwafahamisha Wana YANGA kuhusu mambo muhimu
yaliyomo kwenye Mkataba Huu ulioingiwa kwa kuzingatia na kwa haki miliki
kutolewa kwa Mkodishwaji kwa njia ya Mkataba Huu, kwa kukodisha Timu ya
Soka ya Mmiliki na haki zake zote, mamlaka na majukumu yote, jina lake
na nembo kwa ajili ya kutumika kiamani na kibiashara katika kuziendesha
shughuli za Timu ya Soka ya Mmiliki bila ya kuwa na kuingiliwa katika
muda wa Mkataba huu kwa muda wa Miaka (10) kuanzia Tarehe ya Ufanisi ya
1 Septemba, 2016, ila kama utasitishwa kabla kufuatana na matakwa ya
Mkataba:
3.1 Mkodishwaji
atailipia YANGA deni la Shilingi bilioni kumi na moja na milioni mia
sita na sabini na sita tu (Tshs. 11,676 billioni) inayodaiwa kama
Mmiliki na Mkopeshaji mmoja.
3.2 Mkodishwaji
atailipa YANGA Tshs 100 millioni kwa mwaka ambayo YANGA itawekeza
kiwango kisichopungua (90%) ili kuimarisha mtandao wa Matawi yake.
3.3 Mkodishwaji
atailipa YANGA katika mwaka wa fedha wowote ule kukiwa kuna faida ya
fedha taslim ya asilimia 25% fedha ambayo YANGA itaitumia kujenga uwanja
wake wa mpira.
3.4 Mkodishwaji atalipa hasara za uendeshadji zilizoko katika Mkataba kutoka kwenye mfuko wake bila ya kuweka madai kwa YANGA.
3.5 Mkodishwaji
ataanza kuwekeza kwa vitega uchumi kuanzia siku (90) ya Mkataba katika
mafunzo na vifaa, ambavyo kutakuwepo kiwanja cha mafunzo ya mpira katika
sehemu atakayo ona inafaa kwake yeye Mkodishwaji.
3.6 Mkodishwaji
atahakikisha kuwa majukumu yote ya kifedha ya Timu ya Soka ya YANGA
ikijumlishwa ada ya usajili zinazotakiwa kuanzia Tarehe ya Ufanisi na
majukumu mengine ya siku zijazo yanalipwa kulingana na mahitaji ya YANGA
mapema kutoka kwenye mfuko wa Mkodishwaji.
3.7 Mkodishwaji
atahakikisha kuwa Timu ya Soka ya YANGA haitamaliza chini ya nafasi
nusu mwisho wa msimu wa ligi ya Tanzania Premium League wakati ikiwa
ndani ya kipindi cha Mkataba.
3.8 Mkodishwaji
atahakikisha kuwa Timu ya Soka ya Mmiliki iliyokodishwa katika kipindi
cha misimu 3 mfululizo itamaliza ikiwa ni mshindi wa nafasi 2 za juu
kwenye Tanzania Premium League.
3.9 Mkodishwaji,
kwa kila mwaka atafadhili mashindano ya mpira katika mfumo utakao
amuliwa na yeye Mkodishwaji kwa Timu ya Soka kwa vijana wenye umri chini
ya miaka (18) na kila Tawi la Wanachama wa YANGA litaalikwa kutuma timu
yake kushiriki katika shindano hilo.
3.10 Mkodishwaji
atakabidhi kwa YANGA tuzo zozote au Nishani yoyote Timu ya Soka ya
Mmiliki ikipata, na kuitaarifu YANGA kabla, pale itakapo wezekana, ili
YANGA iweze kumteua mwakilishi wa kupokea tuzo hiyo kwa kuitambua Timu
ya Soka ya Mmiliki.
3.11 Mkodishwaji ataingia katika Mikataba yote ya ufadhili au mikataba yaleseni kwa kuitisha zabuni kupitia Zabuni za Umma.
3.12 Mkodiswaji ataunda na kuiendesha Timu ya Mpira wa Miguu ya vijana kulingana na kanuni na miongozo ya TFF.
3.13 YANGA
itateua moja kati ya kampuni Tano (5) za Ukaguzi Kongwe Duniani wa
Mahesabu zije kukagua kwa kila mwaka hesabu za Mkodishwaji kuhakikisha
hakuna ubadhirifu.
3.14 YANGA
itakuwa na haki ya kipekee kabla ya Tarehe ya Ufanisi wa Mkataba huu
kiwango chochote ambacho kinastahili kupata kutoka TFF, ikiwemo
Mkataba wa Azam TV ambao unakadiriwa kuwa shilingi milioni mia tatu
(300,000,000) kwa matangazo ya msimu uliopita, mikataba ya ufadhili,
madeni ambayo haijalipwa, fedha za zawadi, VAT kutoka TFF na fedha
zingine zote zitapewa umuhimu wa nafasi ya kwanza katika matumizi ya
kukamilisha majukumu ya zamani ya Timu ya Soka ya YANGA ambayo
yalijilimbikiza na hayakuwa wamelipwa.
3.15 Mkataba huu utakapo fikia ukomo, YANGA itakuwa na haki ya kurejesha kile ilichokikodisha.
4. Ilikubaliwa kwamba YANGA:
4.1 Itajitahidi
mnamo kipindi cha miaka miwili ya Mkataba itakuwa na Wanachama hai
100,000 na kwa kila Wanachama 100,000 itateua Mjumbe mmoja kwenye Bodi
ya Wakurugenzi ya Mkodishwaji.
4.2 Itafanya
kila juhudi ya kuongeza ardhi inayohitajika katika Makao Makuu yake
yaliyopo mtaa wa Twiga ili iweze kujenga uwanja wa mpira unaofaa, ambao
Mkodishwaji atawajibika kuchezea michezo yake ya Timu ya Soka ya YANGA,
kwa masharti yatakayo kubaliwa baina ya Pande zote za Wahusika.
4.3 Itakuwa
na haki katika wakati wowote ule ndani ya kipindi cha Mkataba kusitisha
Mkataba ili mradi imfidie Mkodishwaji hasara zote za nyuma, ilipe
malipo yote yaliyofanywa kwa YANGA na Mkodishwaji, inachukua mali
zilizowekezwa na Mkodishwaji na kumfidia mapato ya siku zijazo – zote,
hizi zikiwa zimetathminiwa na moja ya Kampuni za Wakaguzi (5) Kongwe
Duniani.
4.4 Ikiwa
Mkodishwaji atakarabati au atatumia mali yoyote ya YANGA ataifidia
YANGA kwa masharti yaliyokubaliwa kwa masharti tofauti ya Mkataba Huu.
4.5 Mkodishwaji
atakuwa na haki ya kipekee ya kiwakilishi (Exclusive Power of Attorney)
kwa YANGA kufanya mikataba na TFF, CAF & FIFA kwa niaba ya YANGA
bila ya kuingiliwa kati na YANGA lakini anapaswa atoe taarifa kuhusu
uwakilishi huo kwa Baraza la wadhamini, kuanzia Tarehe ya Ufanisi wa
Mkataba Huu pamoja na haki ya uwakilishi wa YANGA kwa: i) kuunda Kamati
zinazohitajika na TFF, CAF na FIFA kuiendesha Timu ya Soka ya Mmiliki
iliyokodishwa ii) kusajili au kulisimamisha benchi la ufundi na
wachezaji kutoka Timu ya Soka ya YANGA, iii) Kuwa Msemaji Mkuu wa Timu
ya Soka ya YANGA kwa Umma.
5. KUFUNGA.
5.1 Bodi
ya Wadhamini wa YANGA inapenda kumshukuru Bw. Yusuf Mehbub Manji kwa
kupendekeza masharti bora kuliko yale yaliyoazimiwa na kukubalika kwa
Wanachama kwa manufaa ya YANGA, na tunampigia saluti uchangiaji wake
usio na choyo kwa manufaa ya YANGA.
5.2 Tungependa
kuufahamisha Umma kwamba Bw. Yusuf Mehbub Manji ametaka kujiuzulu
kutoka Uenyekiti wa Klabu ili kuepusha mgongano wa kimaslahi, lakini
tumelikataa ombi lake hili – kwa vile nafasi ya Mwenyekiti wa Klabu,
Wanachama wameonyesha kwa kura zao kuwa wana imani na uongozi wake, kwa
vile wakati wa majadiliano, haweki maslahi yake binafsi juu ya yale ya
Klabu, lakini anajaribu kadri iwezekanavyo kuisaidia Klabu kuweza
kujitegemea kifedha haraka iwezekanavyo ili kuendelea kushindana katika
mpira wa miguu kwa kiwango cha juu zaidi, hapohapo akilinda urithi wa
Klabu na utamaduni – sifa ambayo tunaihitaji katika Mwenyekiti wa YANGA
na kama akijiuzulu kutoka kwenye Klabu, tutakuwa tumempoteza kiongozi
mwenye uzoefu na maadili ya hali ya juu wakati tunapofanya mageuzi ya
YANGA.
Tunachukua
fursa hii kuwafahamisha Wanachama na Mashabiki kuwa kuna kazi nyingi
kwa faida ya YANGA ambazo Bw. Yusuf Manji anazifanya ambazo hazionekani
mbele ya jamii: kitu ambacho kinahitajika katika Klabu. Tunapenda
kuwafahamisha Wanachama na Mashabiki wawe waangalifu na maneno yao, kwa
vile kauli za maneno ya matusi zinaumiza na zinawavunja moyo viongozi
kama Bw. Yusuf Manji ambao tunafahamu hawagombei nafasi za Uongozi wa
ndani ya Klabu, kwa sababu wanachukizwa na kutukanwa na Wanachama na
hivyo basi, tunawapa mawaidha Wanachama, kwa manufaa ya Klabu watoe
maoni yao kuhusu mambo ya soka na utawala wa soka, na siyo kwa watu na
familia zao.
5.3 Sasa
tunapenda kuwafahamisha Wanachama wa YANGA na Wapenzi wa YANGA kuwa
kilichotiwa saini baina ya Pande Zote ni Mkataba ya kihistoria, na kama
yakitekelezwa na pande zote mbili, YANGA itanufaika kwa hali ya juu mno
kutokana na mazingatio na ushahidi iliyoupata kupitia Baraza lake la
Wadhamini kwenye Mkataba wa ukodishwaji.
5.4 Mwisho,
tumeombwa na Bw. Yusuf Manji tutangaze hadharani Mkataba Huu, hata
hivyo bado tunajadiliana kama kutangazwa huko kutakuwa kwa manufaa ya
Klabu, kwa kuwa, kwa upande mmoja ni vema kuwa na uwazi, lakini kwa
upande mwingine washindani wa Klabu yetu wataiga Mkataba wetu kwa
manufaa yao.
YANGA
DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO
………………………………………….
BODI YA WADHAMINI WA YANGA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni