
Ushindi huo unawafanya Simba wafikishe pointi 23 baada ya kuteremka dimba mara 9 na kujiimarisha kileleni.
Yassin Mzamiru alifunga bao la kwanza akiunganisha kwa kichwa kona iliyochongwa na Shiza Ramadhan.
Shiza Kichuya akaifungia Simba bao la pili kwa penalti dakika ya 73 beki wa Kagera Sugar, Juma Ramadhan kumkwatua Mohamed Ibrahim ndani ya eneo la hatari.
Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa; Vincent Angban, Janvier Bokungu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murshid, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shizza Kichuya, Muzamil Yassin, Frederick Blagnon/Laudit Mavugo dk56, Ibrahim Hajib/Mohammed ‘Mo’ Ibrahim dk60 na Mwinyi Kazimoto/Said Ndemla dk84.
Kagera Sugar; Hussein Sharrif ‘Cassilas’, Mwahita Gereza, Godfrey Taita, Juma Ramadhan, George Kavilla, Suleiman Mangoma, Ally Nassoro, Shaaban Sunza, Danny Mrwanda/Themi Felix dk62, Edward Christopher/Paul Ngway dk62 na Mbaraka Abeid/Ally Ramadhani dk38.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni