STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 12 Oktoba 2016

SIMBA YAUNGURUMA SOKOINE, CHIRWA ATOA MKOSI MTIBWA AKIFA TAIFA, AZAM TAABANI SHINYANGA

Wekundu wa Msimbazi Simba SC wakiwa jijini Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine kucheza na wenyeji wao Mbeya City wameendeleza wimbi la ushindi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Simba walionekana kuwa na dalili za kuibuka na ushindi mapema tu baada ya washambulizi wake Ibrahim Ajibu, Shiza Kichuya na Fredrick Blagnon kulisakama lango la Mbeya City mithili ya nyuki.

Iliwachukua dakika sita tu tangu filimbi ya mwamuzi ipulizwe Simba kupata bao kupitia kwa Ibrahim Ajibu 'Fundi', ambaye alipiga mpira wa adhabu mujarab na kutinga moja kwa moja wavuni,

Ajibu aliendelea tena kulikasakama lango la Mbeya City baada ya kuachia shuti kali dakika ya 15 lakini mpira uligonga mwamba na kurudi uwanjani kabla ya kuokolewa na walinzi wa Mbeya City.

Simba walipata penati baada ya Blagnon kufanyiwa madhambi na kupiga mwenyewe lakini alikosa baada ya kipa wa Mbeya City kupangu mpira.

Kiungo mshambuliaji wa pembeni wa Simba aliye kwenye kiwango bora kwa sasa, Shiza Kichuya alifunga bao la pili mnamo dakika ya 33 baada ya kumhadaa beki wa Mbeya City na kuupiga mpira kwa ufundi wa hali ya juu ya kuandika bao lake la sita msimu huu akiwa ndio kinara wa mabao.

Kikosi cha Simba kilikuwa; Vincent Agban, Janvier Bukungu, Mohammed Hussein 'Tshabalala', Method Mwanjali, Novart Lufunga, Mkude Jonas, Muzamil Yassin, Kazimoto Mwinyi Kichuya, Shiza Kichuya, Frederick Blagnon na Ibrahim Hajib.

Mbeya City; Owen Chaima, John Kabanda, Michael Kerenge, Tumba Swedi, Rajab Zahir, Sankhani M, Joseph Mahundi, Kennu Ally, O Ramadhani, Raphael Daudi na Ditram Nchimbi.

Kule jijini Dar

Mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa amefunga goli lake la kwanza tangu alipotua kwenye klabu hiyo kabla ya msimu huu kuanza alipojumuishwa kwenye kikosi cha Jangwani kikiwa kwenye michuano ya Caf.

Chirwa alifunga goli lake la kwanza kwenye msimu huu ikiwa ni mechi ya saba kwa Yanga katika ushindi wa mabao 3-1

Mzambia huyo aliunganisha mpira uliochelewa kuokolewa na mabeki baada ya kupigwa kona iliyookolewa lakini mpra ukamkuta mfungaji ambaye alipiga fataki kali nakutinga

Chirwa alifunga bao hili dakika ya 45 na kuifanya timu yake kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa Mtibwa kutulia na kusawazisha bao safi kupitia kwa Haruna Chanongo baada ya kutumia vyema uzembe wa mabeki wa Yanga Kelvin Yondani na Adrew Vincent 'Dante'

Yanga walikuja juu na kuongeza bao la pili kupitia kwa Simon Msuva aliyeambaa na mpira winga ya kulia na kuingia eneo la hatari na kupiga shuti kali lililoingia moja kwa moja.

Donald Ngoma aliyeingia kutoka benchi kuchukua nafasi ya Chirwa aliifungia Yanga bao la tatu baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Geoffrey Mwashiuya kutoka kushoto mwa uwanja.

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Vincent Andrew, Kevin Yondan, Said Juma ‘Makapu’/Mbuyu Twite dk74, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Amisi Tambwe, Obrey Chirwa/Donald ngoma dk73 na Deus Kaseke/Geoffrey Mwashiuya dk46.
Mechi za leo 2016-10-12
FT
MBEYA CITY
0
 : 
2
SIMBA SC
FT
MWADUI FC
2
 : 
0
African Lyon
FT
MBAO FC
3
 : 
1
TOTO AFRICANS
FT
MAJIMAJI
0
 : 
1
KAGERA SUGAR
FT
YANGA
3
 : 
1
MTIBWA SUGAR
FT
STAND UNITED
1
 : 
0
Azam FC
FT
JKT RUVU
0
 : 
0
T.PRISONS
MICHEZO INAYOKUJA
2016-10-13
16:00
RUVU SHOOTING
Vs    
NDANDA FC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox