Leo kwenye mwendelezo wamechi za Ligi Kuu Tanzania Bara jumla ya mechi sita zimechezwa kwenye viwanja tofauti huku macho na masikio ya wengi yakiwa kwenye mechi tatu za vigogo Simba, Yanga na Azam.
Yanga wameweza kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Prison katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Prisons itabidi wajilaumu wenyewe baada ya kuwa wa kwanza kupata
penati lakini wakashindwa kuitumia baada ya kipa wa Yanga Benno
Kakolanya kuipangua na kuokolewa na mabeki wa Yanga.
Simon Msuva aliifungia Yanga bao la pekee na la ushindi kwa njia ya
penati mnamo dakika ya 73 baada ya Obrey Chirwa kuangushwa ndani ya
eneo la hatari.
Katika dimba la Uhuru, vinara Simba wamepoteza rekodi yao ya
kutopoteza mchezo msimu huu baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka
kwa African Lyon.
Abdallah Mguhi alikuwa shujaa wa African Lyon kwa bao lake la
dakika ya mwisho kabisa ya muda wa nyongeza ambalo limewapunguza Simba
kasi.
Katika uwanja wa CCM Kirumba, wenyeji Mbao wameondoka na pointi tatu baada ya kuwachapa Azam kwa mabao 2-1.
Mabao ya washindi yalifungwa na Venance Ludovic dakika ya 30 na
Boniphace Maganga dakika ya 50 huku lile la kufutia machozi la Azam
likifungwa na Francesco Zekumbawira dakika ya 67.
Matokeo kwenye mechi zingine ni JKT Ruvu imetoka sare ya mabao 1-1
na Toto africans, wakati Nanda imeichapa Stand United 2-1 na Kagera
Sugar ikiwatandika Ruvu shooting 3-1
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni