HATMA ya
mfanyabiashara Mohamed Dewji 'MO' kutaka kununua hisa za klabu ya Simba
kwa asilimia 51 sasa itajulikana Disemba 11 baada ya uongozi kuitisha
Mkutano Mkuu wa dharura, mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa Bwalo
la Maafisa wa Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Kamati ya
Utendaji ya klabu hiyo ilikutana juzi Novemba 18 chini ya Rais, Evans
Aveva na kupitisha kwa kauli moja mkutano huo wa mabadiliko ya katiba
ambao utaruhusu MO kuwekeza Sh 20 bilioni kama alivyotamka hapo awali.
Kamati ya
Utendaji ina mamlaka ya kuitisha mkutano huo kwa mujibu wa Katiba ya
Simba Ibara ya 22 kifungu cha kwanza ambapo nyaraka za mkutano huo
zitatolewa kwa wanachama wao kupitia matawi yote ya Simba kwa muongozo
wa Ibara ya 22 kifungu cha nne cha Katiba yao.
Septemba,
Baraza Michezo la Taifa (BMT) kupitia Katibu mkuu Mohamed Kiganja
lilipiga marufuku kwa klabu za Simba na Yanga kufanya mabadiliko ya
kiundeshaji hadi hapo zitakapofuata taratibu kwa mujibu wa Katiba zao
ambapo sasa Wekundu hao wameanza kufuata maelekezo hayo.
Hata hivyo
Kiganja, amesisitiza kuwa, Katiba ya Simba iliyopo na inayotambuliwa
kwa msajili ni ile ya 2010 ambayo ina mapungufu mengi hivyo wanapaswa
kuwa makini na ili mchakato huo ukamilike na kupitishwa ni lazima
msajili wa vyama vya michezo aikubali na kugonga mhuri na si vinginevyo.
"Wafanye
mkutano wao maana kila kitu kipo wazi, utaratibu unajulika na mabadiliko
ya Katiba nayo si jambo la mara moja hivyo taratibu zifuate na mengine
yatafuata," alisema Kiganja.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Jumatatu, 21 Novemba 2016
MABADILIKO YANUKIA MSIMBAZI, MO MBIONI KUKABIDHIWA TIMU
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni