AGUERO AFUNGIWA MECHI
NNE.
MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Sergio Aguero amefungiwa kutocheza
mechi nne baada ya kutolewa kwa mara ya pili kwa kadi nyekundu msimu
huu. Aguero mwenye umri wa miaka 28, alitolewa nje kwa kumchezea vibaya
beki wa Chelsea David Luiz katika mchezo wa Jumamosi iliyopita ambao
walifungwa mabao 3-1. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina Agosti mwaka
huu pia alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya Winston
Reid wa West Ham United. Aguero sasa anatarajiwa kukosa mechi za City
watakazocheza na Leicester City, Watford, Arsenal na Hull City. Kiungo
wa City Fernandinho ambaye naye pia alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya
kuzozana na Cesc Fabregas kufuatia tukio la Aguero, yeye amefungiwa
kucheza mechi tatu.
Today Deal $50 Off : https://goo.gl/efW8Ef
Today Deal $50 Off : https://goo.gl/efW8Ef
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni