STORI MCHANGANYIKO DECEMBER 7;
STORI YA KWANZA;
MAREFA waliochezesha mchezo namba 49 kati ya Yanga na Simba, Martin Saanya na Samweli Mpenzu wametolewa kwenye ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, huku suala lao likipelekwa kwenye Kamati ya Waamuzi ili ishughulikie tatizo lao kitaalam.
Maamuzi
hayo yamefanyika baada ya Kikao cha Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji
ya Bodi ya ligi, kuwaita na kuwahoji na kuangalia mkanda wa mchezo
husika. Kamati imebaini mapungufu mengi ya kiutendaji yaliyofanywa na
waamuzi hao, na hivyo kuitaka kamati ya waamuzi ishughulikie.
Pia
Mwamuzi Rajabu Mrope aliyechezesha mchezo namba 108 kati ya Mbeya City
na Yanga naye ametolewa kwenye Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom msimu
2016/2017 na kurudishwa kwenye Kamati ya Waamuzi ili waweze kumpangia
daraja lengine la uamuzi.
Martin Saanya (kulia) amefutwa katika orodha ya waamuzi wa Ligi Kuu
Mrope alitiwa hatiani kwa kosa la kutojiamini mchezoni na kwenye uamuzi wake na kushindwa kuudhibiti mchezo.
Miongoni mwa matatizo ya mwamuzi huyo ni kukubali goli, kisha kukataa na mwisho kukubali tena hali iliyoonyesha kutokujiamini na kusabisha mtafaruku mkubwa katika mchezo huo.
Katika ligi ya Daraja la kwanza, Mwamuzi Thomas Mkombozi aliyechezesha mechi namba 15B kati ya Coastal Union na KMC ameondolewa kwenye orodha ya waamuzi kutokana na kushindwa kuudhibiti mchezo na kutoshirikiana na wasaidizi wake.
Adhabu hiyo ametolewa baada ya Kamati ya usimamizi na uendeshaji wa ligi kuwaita waamuzi wa mchezo huo na kufanya mahojiano nao na kugundua Mkombozi alikuwa na maamuzi mengi bila umakini na hakushirikiana kiufundi na wasaidizi wake. Kutokua makini kulisababisha mchezo huo kumalizika kwa vurugu.
Pia Klabu ya Coastal Union imepewa adhabu ya kucheza bila ya mashabiki kwa mechi mbili za nyumbani na mechi moja ya nyumbani kuchezwa uwanja wa ugenini kwa kosa la mashabiki wa timu hiyo kumshambulia Mwamuzi Thomas Mkombozi na kumsababishia majera ha maumivu makali.
kuhusu Mwamuzi Ahmed Seif, Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji ya bodi ya Ligi, imemfungulia na kumtoa kwenye orodha ya waamuzi wa Ligi kuu mwamuzi huyo aliechezesha mchezo namba 28 kati ya African Lyon na Mbao FC. hivyo, Mwamuzi Ahmed Seif atarudishwa kwenye kabati ya waamuzi ili apangiwe majukumu mengine.
STORI YA PILI;
SIMBA SC inatarajiwa kushuka dimbani Desemba 12, mwaka huu Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kumenyana na Power Dynamos ya Zambia.
Mchezo huo utakaochezwa siku ya sherehe za Maulid kuazimisha kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W.) ni maalum kwa kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog kumjaribu kipa mpya, Daniel Agyei kutoka Medeama SC ya Ghana.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Hajji Sunday Manara amesema leo mjini Dar es Salaam kwamba kikosi cha timu hiyo kinaendelea na mazoezi mjini Morogoro.
Manara amesema kwamba kikosi kitawasili Dar es Salaam asubuhi ya kuamkia mchezo huo, Jumatatu – na baada ya hapo kitaendelea na maandalizi ya mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu ya Vodacom Tnzania Bara mzunguko wa pili dhidi ya Ndanda FC mjini Mtwara.
Wachezaji wa Simba waliopo kambini Morogoro ni makipa; Vincent Angban, Peter Manyika, Daniel Agyei, na Dennis Richard, mabeki; Hamad Juma, Janvier Bokungu, Abdi Banda, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Emmanuel Semwanza, Malika Ndeule, Novaty Lufunga na Method Mwanjali.
Viungo ni Awadh Juma, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Said Ndemla, Mussa Ndusha, Muzamil Yassin, Jamal Mnyate, Shizza Kichuya na washambuliaji Frederick Blagnon, Laudit Mavugo, Ame Ally na Ibrahim Hajib na Hajji Ugando.
Mchezaji pekee anayekosekana Simba kwa sasa ni beki Mganda, Juuko Murshid, ambaye ana ruhusa maalum, yupo na timu yake ya taifa inayojiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Gabon mwezi ujao.
Simba ilimaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara katika nafasi ya kwanza kwa pointi zake 35, mbili zaidi ya mabingwa watetezi, Yanga.
Wakati huo huo: Baraza la Wazee la Simba SC limewahimiza wanachama wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi katika mkutano wa kubadilisha Katiba Jumapili ya Desemba 11, mwaka huu ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam.
Hata hivyo, mkutano huo umepingwa na Baraza la Wadhamini la klabu, lililoelekeza taratibu kadhaa zifuatwe kwanza, ikiwemo uhakiki wa wanachama chini ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
STORI YA TATU;
Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Young Africans, wameamua kuachana na Mbuyu Twite na nafasi yake kuchukuliwa na Justine Zulu.
“Justine Zulu ametafutwa baada ya kujua kwamba mkataba wa Mbuyu Twite unaisha mwezi Disemba, Mkataba wa Twite umeisha na nafasi yake imechukuliwa na Justine Zulu,” Baraka Deudedith akijibu kuhusu hatma ya Mbuyu Twite ndani ya kikosi cha Yanga.
Ujio wa Zulu kwenye kikosi cha Yanga uliongeza idadi ya wachezaji wa kigeni hadi kufikia nane (8) inyume na sheria na kanuni za ligi kuu Tanzania bara ambapo vilabu husika vinapaswa kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi saba (7).
Kwa hiyo moja kwa moja kanuni ziliitaka Yanga kupunguza mchezaji mmoja ambapo Mbuyu ikabidi apishe nafasi nafasi.
Kumekuwa na minong’ono kwamba huenda mchezaji huyo kiraka akajiunga na Simba SC. Lakini jana uongozi wa Simba kupitia manager wake Musa Hassan ‘Mgosi’ alikanusha taarifa za klabu yake kutaka kumsajili Mbuyu Twite.
KIMATAIFA;
TOP 20 YA WACHEZAJI WANAOLIPWA MKWANJA MREFU EPL;
1: PAUL POGBA (MAN UTD)
£290,000 kwa wiki mpaka 2021
2: WAYNE ROONEY (MAN UTD)
£260,000 kwa wiki mpaka 2019
3: ZLATAN IBRAHIMOVIC (MAN UTD)
£250,000 kwa wiki mpaka 2017
4: SERGIO AGUERO (MAN CITY)
£240,000 kwa wiki mpaka 2019
5: YAYA TOURE (MAN CITY)
£220,000 kwa wiki mpaka 2017
6: EDEN HAZARD (CHELSEA)
£200,000 kwa wiki mpaka 2020
7: DAVID SILVA (MAN CITY)
£200,000 kwa wiki mpaka 2019
8: DAVID DE GEA (MAN UTD)
£185,000 kwa wiki mpaka 2019
9: RAHEEM STERLING (MAN CITY)
£180,000 kwa wiki mpaka 2020
10. KEVIN DE BRUYNE (MAN CITY)
£170,000 kwa wiki mpaka 2021
11. CESC FABREGAS (CHELSEA)
£170,000 kwa wiki mpaka 2019
12. MESUT OZIL (ARSENAL)
£140,000 kwa wiki mpaka 2018
13. JUAN MATA (MAN UTD)
£140,000 kwa wiki mpaka 2018
14. BASTIAN SCHWEINSTEIGER (MAN UTD)
£135,000 kwa wiki mpaka 2018
15. ALEXIS SANCHEZ (ARSENAL)
£130,000 kwa wiki mpaka 2018
16. DIMITRI PAYET (WEST HAM)
£125,000 kwa wiki mpaka 2021
17. WILLIAN (CHELSEA)
£120,000 kwa wiki mpaka 2020
18. VINCENT KOMPANY (MAN CITY)
£120,000 kwa wiki mpaka 2019
19. DANIEL STURRIDGE (LIVERPOOL)
£120,000 kwa wiki mpaka 2019
20. THIBAUT COURTOIS (CHELSEA)
£120,000 kwa wiki mpaka 2019
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni