STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 21 Desemba 2016

BREAKING; VIONGOZI SIMBA,YANGA NA AZAM WAMEKAMATWA NA IDARA YA UHAMIAJI....


Image result for idara ya uhamiaji tanzania


IDARA ya Uhamiaji leo imewakamata viongozi wa klabu za Azam, Simba na Yanga kwa makosa tofauti ya kuajiri na kuwatumikisha wageni bila kuwa na vibali.
Image result for SIMBA,YANGA NA AZAM

Habari za ndani ambazo tumezipata zinasema kwamba waliokamatwa ni Mtendaji Mkuu wa Azam, Saad Kawemba na Makatibu Wakuu wa Simba, Patrick Kahemele na Yanga Baraka Deusdedit.


Kwa pamoja wote wanakabiliwa na tuhuma za kuwaruhusu wachezaji na makocha wao wa kigeni kufanya kazi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mwishoni mwa wiki bila na vibali.




Upande wa Azam wanaodaiwa kucheza bila kuwa na vibali ni beki Yakubu Mohammed, washambuliaji Yahaya Mohammed, Samuel Afful wote kutoka Ghana na kiungo mkabaji Stephan Kingue Mpondo kutoka Cameroon.

Kwa Simba wanaodaiwa kucheza bila kuwa na vibali ni kipa Daniel Agyei na kiungo James Kotei, wakati Yanga inatuhumiwa kuwatumia makocha wake, George Lwandamina na Noel Mwandila wakiwa hawana vibali.


Kiungo mpya wa Yanga, Justin Zulu hakucheza mwishoni mwa wiki na alikuwa jukwaani.


Bin Zubeiry Sports – Online inaendelea kumtafuta Msemaji wa Idara ya Uhamiaji kwa taarifa zaidi. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox