MSHAMBULIAJI wa zamani wa Manchester United, Carlos Tevez anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake wa fedha nyingi kwenda China licha ya mashabiki wa Boca Juniors kumuomba kwa hisia kali jana usiku shujaa wao abaki.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 32 na mshambuliaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Argentina anatarajiwa kusaini mkataba na klabu ya Ligi Kuu ya China, Shanghai Shenhua kwa mshahara wa Pauni 615,000 kwa wiki.
Na mchezaji huyo wa zamani wa West Ham, Manchester United na Manchester City alitumia fursa hiyo kuwaaga mashabiki wa klabu yake ya kwanza kuchezea wakiifunga Colon mabao 4-1 huko La Bombonera.
Akiwa amefunga bao la pili siku hiyo, Tevez alitolewa dakika ya 90 kupewa fursa ya kuwaaga mashabiki majukwaani.
Shabiki mmoja alimkimbilia Tevez uwanjani na kumpigia magoti akimsihi asiondoke, kabla ya kuondolewa na walinzi.
Majukwaani mashabiki walionyesha upendo mkubwa kwa Tevez wakiwa wamebeba mabango yenye kusomeka; 'usiondoke Carlos!'
Tevez
atakuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani Pauni 615,000 kwa wiki ni
sawa Pauni Milioni 31.98 kwa mwaka na aatafutaiwa na Mbrazil Oscar wa
Shanghai SIPG anayelipwa Pauni 400,000 kwa wiki, Cristiano Ronaldo wa
Real Madrid Pauni 365,000 kwa wiki, Lionel Messi wa Barcelona Pauni
365,000 kwa wiki na Gareth Bale wa Real Madrid Pauni 346,000 kwa wiki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni