STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 24 Desemba 2016

SIMBA WAONGEZA GEPU LA POINTI KILELENI HADI MWAKANI, WAICHAPA JKT RUVU 1-0



Vinara wa ligi kuu ya vodacom Simba SC wameongeza tofauti ya pointi kati yao na mabingwa watetezi Yanga kutoka pointi moja mpaka pointi 4 baada ya leo kuibuka na ushindi wa goli 1-0 mbele ya JKT Ruvu mchezo uliochezwa katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.

Mechi hiyo iliyochezeshwa na Hans Mabena wa Tanga aliyesaidiwa na Omar kambangwa wa Dar es Salaam na Khalfan Sika wa Pwani,

Katika mchezo huo uliokuwa wa kasi na kushambuliana kwa zamu Simba SC iliwabidi kungoja mpaka dakika ya 45 kuandika goli pekee la mchezo huo lililofungwa na Mzamiru Yassin kunako dk ya 49, aliyemalizia krosi ya Pastori Athanas baada ya kipa wa JKT Ruvu kuanguka chini baada ya kuoka mpira.

Katika kipindi cha pili Simba SC walitengeneza nafasi nyingi ukilinganisha na kipindi cha kwanza lakini safu yake ya ushambuliaji ilishindwa kuzitumia nafasi hizo.

JKT Ruvu nao hawakuwa nyuma katika kutengeneza nafasi, ambazo nao walishindwa kuzitumia na kupeleekea mchezo kumalizika kwa Simba SC kushinda goli 1-0.
Kwa ushindi huo, Simba inafikisha pointi 42 baada ya kucheza mechi 17 huku wakifatiwa na Yanga yenye point 37

Kikosi cha Simba kilikuwa: Daniel Agyei, Jonas Mkude, Janvier Bukungu/Hamad Juma dk50, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Abdi Banda, Method Mwanjali, Shiza Kichuya, James Kotei/Said Ndemla dk79, Pastory Athanas na Mohamed Ibrahim/Jamal Mnyate dk62. 

JKT Ruvu: Hamis Seif, Salim Gilla, Michael Aidan, Frank Nchimbi, Yussuf Chuma, Kelvin Nashon, Edward Joseph, Hassan Dilunga, Hassan Materema, Mussa Juma/Kassim Kisengo dk80 na Ally Bilal/Atupele Green dk62.

MATOKEO MENGINE KUNAKO VPL
1. Majimaji 1-1 Azam FC
wafungaji katika mchezo huo ni  Yahay Muhammed kwa upande wa Azam FC na Kondo Alex kwa upande wa Majimaji.
2.kagera sugar 1-0  Stand United
Mfungaji ni Mbaraka Yusuph
3.Ndanda 0-2 Mtibwa Sugar
Wafungaji ni vicent barnabas na Haruna Chanongo
4.Mwadui 1-0 Mbao
Mfungaji Awadh Juma
5. Mbeya city 0-0 Toto Africa


Msimamo wa Ligi Kuu Msimu Huu

RnTimuPWDLFAGdPts
1SIMBA SC1713222962341
2YANGA1711423592637
3KAGERA SUGAR178451716128
4Azam FC177642415927
5MTIBWA SUGAR177642219327
6STAND UNITED175751514122
7T. PRISONS165741010022
8MBEYA CITY175661315-221
9Ruvu Shooting164841517-220
10African Lyon174761116-519
11MWADUI FC175481421-719
12NDANDA FC175481320-719
13Mbao FC175391621-518
14MAJIMAJI FC1752101325-1217
15TOTO AFRICANS173410918-913
16JKT RUVU17278616-1013


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox