Mabingwa wa soka Tanzania bara Dar es salaam Yanga African wamelazimishwa sare
ya bao moja dhidi ya African Lyon mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa
Uhuru na kushindwa kuishusha Simba kileleni.
Matokeo
hayo yanaifanya Yanga iendelee kukamata nafasi ya pili kwa pointi zake
37 baada ya kucheza mechi 17 sawa na Simba iliyo kileleni kwa pointi
zake 38. Simba inaweza kuongeza gepu la pointi hadi nne iwapo itashinda
dhidi ya JKT Ruvu leo Uwanja wa Uhuru.
Hadi
mapumziko hakuna timu iliyofanikiwa kupata bao na African Lyon
walicheza kwa kujihami zaidi kipindi cha kwanza wakifanya mashambulizi
ya kushitukiza
Mchezo huo ulikuwa wa taratibu ambapo
dakika 45 za kipindi cha kwanza hakukuwa na shambulizi lolote la hatari
kwa pande zote mbili licha ya Yanga kumiliki sehemu kubwa ya mchezo.
Mlinda mlango wa Yanga Deogratius
Munishi 'Dida' kwa muda mrefu wa kipindi hicho alikuwa likizo kutokana
na kukosekana kwa kashkashi baada ya Lyon kucheza zaidi nyuma na
katikati ya uwanja.
Ludovic Venance aliipatia Lyon bao
dakika ya 58 baada ya kupokea pasi ya Abdallah Mguhi ambaye alikuwa
mwiba mkali upande wa kushoto ambao Haji Mwinyi alishindwa kabisa
kumdhibiti.
Tambwe aliisawazishia Yanga kwa
kichwa dakika ya 74 baada ya kumalizia krosi ya beki Juma Abdul kutokana
na Lyon kushindwa kuokoa mpira ambao ulionekana hauna madhara.
Lyon iliwatoa Awadh Juma, Omari
Abdallah na Thomas Morice na kuwaingiza Ludovic, Peter Mwalyanzi pamoja
na Cosmas Lewis. Yanga iliwapumzisha Thaban Kamusoko, Mwinyi na Deus
Kaseke na kuwaingiza Gofrey Mwashiuya, Emanuel Martin na Obrey Chirwa.
Yanga imefikisha pointi 37 alama moja
nyuma ya Simba ambao kesho watacheza na JKT Ruvu na endapo watashinda
wataongeza 'gepu' la pointi kufikia nne.
Kikosi
cha African Lyon kilikuwa; Youthe Jehu, Baraka Jaffary, Miraji Adam,
Halfan Twenye, Hamad Wazir, Hamad Manzi, Hassan Isihaka,Omary
Abdallah/Peter Mwalyanzi dk80, Awadhi Juma/ Ludovic Venance dk46, Thomas
Maurice/Cossmas Lewis dk82. na Abdallah Mguhi.
Yajnga
SC; Deogratias Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Haruna Niyonzima, Mwinyi
Hajji Mngwali/ Geoffrey Mwashiuya dk74, Kelvin Yondan, Vincent Bossou,
Simon Msuva, Thabani Kamusoko/ Obren Chirwa dk56, Amissi Tambwe, Said
Juma na Deus Kaseke/ Emanuel Martin dk65.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Ijumaa, 23 Desemba 2016
VPL; BAADA YA KUMALIZA MGOMO, YANGA WAGAWANA POINTI NA AFRICAN LYON
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni