Kamati
ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) imemaliza kikao chake na Simba inaendelea kubaki na pointi
ilizopewa na Kagera Sugar.
Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Celestine, amesema kamati hiyo itakaa tena na kuna shahidi wengine wataitwa kuhojiwa.
Kikao
hicho kimefanyika kuanzia leo asubuhi katika hoteli ya Protea jijini
Dar es Salaam na waamuzi, wafanyakazi wa bodi ya ligi, viongozi wa
simba, Kagera Sugar, waamuzi wa mechi kati ya Kagera Sugar dhidi ya
African Lyon na beki Mohammed Fakhi wamehojiwa.
Baada
ya kuhojiwa, kilichofuatia lilikuwa ni suala la kamati kukaa kwa
takribani saa moja kuonyesha walikuwa wakimalizia kuhusiana na kile
walichowahoji wahusika.
Kabla, kamati ya Saa 72, ilikuwa imeipa Simba pointi tatu na mabao matatu licha ya kufungwa kwa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar.
Kamati
ya Saa 72, ilibaini Kagera Sugar ilimchezesha Fakhi mechi hiyo kwenye
Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba akiwa na kadi tatu za njano.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni