
Rukyaa alikuwa refa wa akiba katika mchezo huo ambao inadaiwa Fakih alipata kadi nyingine ya njano kukamilisha tatu dhidi ya African Lyon Jumatano ya Januari 18, 2017 uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba amefuta utata.
“Rukyaa ametoa ushahidi wake ambao umefanana na wa Kamisaa, kwamba Fakih hakupewa kadi ya njano Januari 18. Na muda ambao refa anasema alimuonyesha kadi ya njano tayari alikuwa amekwishatoka uwanjani baada ya kuumia,” kimesema chanzo kutoka kwenye kikao cha Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF kinachoendelea hivi sasa hoteli ya Courtyard, katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
Katika barua iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Kagera Sugar, Hamisi Madaki kuelekea kwa Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa, klabu hiyo imeliomba shirikisho hilo kupitia upya maamuzi ya Kamati ya Saa 72 kwa kuwa Fakhi hakuwa na kadi tatu za njano kama ilivyodaiwa.
Ikumbukwe Simba iliwasilisha malalamiko ikitaka ipewe ushindi wa pointi tatu na mabao matatu kutokana na Kagera Sugar kumchezesha Fakhi akiwa na kadi tatu za njano katika mechi yao namba 194 iliyofanyika Aprili 2, 2017 Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
CHANZO: www.binzubeiry.co.tz
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni