STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 15 Aprili 2017

SIMBA WAENDELEZA REKODI MBOVU MBELE YA TOTO,MBIO ZA UBINGWA BADO MBICHI........



SARE ya bila kufungana waliyoipata Toto African dhidi ya Simba imefanya mbio za ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara kuendelea kuwa wazi ambapo kama mabingwa watetezi Yanga wakishinda michezo yake miwili ya kiporo watarejea kileleni mwa msimamo huo.

Simba imefikisha pointi 62 alama sita mbele ya Yanga walio katika nafasi ya pili wakiwa na tofauti kubwa ya magoli ya kufunga na kufungwa sifa itakayowafanya waweke makazi kileleni endapo tu watawafikia Simba kwa pointi.

Katika mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Simba ilishindwa kutengeneza nafasi nyingi nzuri kutokana na ubovu wa mipango yao hasa eneo la kiungo.

Straika Fredrick Blagnon ambaye mchezo uliopita dhidi ya Mbao FC alikuwa shujaa kwa kufunga mabao mawili leo alishindwa kufurukuta licha ya kupata nafasi mbili za wazi kipindi cha kwanza ambazo alishindwa kuzitumia huku safu ya ulinzi ya Toto ikionekana kutulia hali iliyopelekea Simba kuondoka na alama moja.
 Jamal Simba Mnyate wa Simba akiwania mpira na beki wa Toto Africans
Wekundu hao wamemaliza michezo yao ya kanda ya ziwa ambapo sasa watarejea jijini Dar es Salaam kumalizia mechi tatu zilizobaki ambazo zitafanyika kwenye uwanja wa Taifa.

Katika miaka saba iliyopita Simba haijawahi kuifunga Toto katika uwanja wa CCM Kirumba.

Kwa upande mwingine, mshambuliaji Abdulrahaman Mussa amefunga hat trick ya pili msimu huu alipofunga mabao matatu leo katika ushindi wa mabao 4-1 wa Ruvu Shooting dhidi ya Majimaji.

Kelvin Sabato alifunga hat trick ya kwanza msimu huu alipoifunga Mtibwa Sugar mabao matatu kwenye sare ya mabao 3-3 iliyopata Stand United.

Matokeo:
Toto Africans 0-0 Simba
Ruvu Shooting 4-1 Majimaji
Stand United 0-0 Mtibwa Sugar
 JKT Ruvu 2-2Azam 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox