Awali Mo alikaririwa akisema amejiengua katika masuala yote yanayohusu klabu hiyo ukiwemo mpango wake wa kuwekeza klabuni kwa mabilioni ya shilingi baada ya kutoshirikishwa katika makubaliano ya mkataba huo huku akitaka pia kurudishiwa kiasi cha pesa alichokuwa amewakopesha.
Mmoja wa viongozi wa klabu hiyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe kwenye mtandao huu amesema kwa sasa wamemaliza tofauti zao na Mo na amerejea klabuni hapo huku mchakato wa kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo ukiendelea.
“Tulikuwa na kikao cha pamoja na Mo kujadili kuhusu suala la mkataba tulioingia na SportPesa, ni kwamba tumeelewana na amerejea kundini jambo ambalo ni zuri kwa mustakabali wa klabu,” alisema kiongozi huyo.
Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya usajili na mjumbe wa kamati ya Utendaji ya klabu hiyo Zacharia Hanspope kurejea kundini baada ya hapo awali kutangaza kujiuzulu nafasi hizo kwa sababu zilielezwa kuwa ni kutokubaliana na baadhi ya mambo katika mchakato huo.
Mei 27 timu ya Simba itacheza mchezo wa fainali wa kombe la FA dhidi ya Mbao FC na endapo itaibuka na ushindi itaiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika hapo mwakani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni