
Game ya Man United ilimalizika kwa sare ya kufungana 1-1 goli la Man United likifungwa na Fellaini dakika ya 17 na goli la Celta Vigo lilifungwa dakika ya 85 na Roncaglio, sare hiyo imeiwezesha Man United kuingia hatua ya fainali baada ya mchezo wa kwanza kuifunga Celta Vigo goli 1-0 ugenini.

Mchezo wa fainali ya UEFA Europa League itachezwa katika uwanja wa Friends mjini Stockholm nchini Sweden May 23 2017, hii inakuwa ni mara ya pili kwa kocha wa Man United Jose Mourinho kufanikiwa kufikia hatua ya fainali ya michuano hiyo akiwa na timu mpya katika msimu wa kwanza, mara ya kwanza ilikuwa 2002/03 akiwa na FC Porto ya kwao Ureno.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni