STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 27 Machi 2018

TAIFA STARS KANYAGA TWENDE , WAICHEZESHA NDOMBOLO WAKONGO PALE TAIFA, SAMATA KICHUYA WAUWAJI

Timu ya soka ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya DR Congo (The Leopards) katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Wakicheza kandanda safi na la kuvutia mbele ya umati wa Watanzania, Taifa Stars walipata Mabao yote katika kipindi cha pili kupitia kwa Nahodha Mbwana Samatta na Shiza Kichuya.

Dakika ya nne shuti la Shiza Kichuya baada ya kupokea Mpira uliopanguliwa na kipa wa DR Congo Ley Matampi Lakini shuti lake likaota mbawa na kuwa goal kick.

Stars wakicheza soka la kuvutia waliendelea kupanga mikakati ya kuipita ngome ya DR Congo wakiwatumia wachezaji Shiza Kichuya, Simon Msuva, Mbwana Samatta na Mohammed Issa.

Aidha katika dakika ya 25 almanusura waandike bao la kuongoza baada ya Mbwana Samatta kuwatambuka mabeki wa DR Congo na kumpatia pasi Gadiel Michael ambaye alipiga shuti kali lakini lilipanguliwa vizuri na kipa Ley Matampi.
Stars waliendelea kulikaribia Lango la DR Congo kila mara ambapo katika dakika ya 37 Simon Msuva alipata nafasi ya kuiweka mbele Stars lakini kichwa chake hakikulenga lango la Congo.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna timu ambayo ilikuwa imepata bao, kipindi cha Tanzania walikuja kwa kasi na kama sio kukosa umakini kwa mwamuzi Elly Sassi basi Taifa Stars wangepata penati baada ya Simon Msuva kuonekana dhahiri shairi kusukumwa wakati akijaribu kufunga.

Kadhalika katika dakika ya 51 Taifa Stars walikosa tena nafasi ya kuandika bao la kuongoza baada shuti la Msuva akitokea pembeni mwa lango la DRC kugonga nyavu ndogo.
Mwalimu Mayanga alifanya mabadiliko katika dakika ya 59 kwa kumtoa Mohamed Issa ambaye alipata majeraha na kumuingiza Ibrahim Ajib Migomba kuziba nafasi yake.

Dakika ya 74 Mpira ulioanzia kwa Kelvin Patrick Yondani na kumkuta Simon Msuva naye bila uchoyo akampa Shiza Kichuya na yeye akapiga Krosi tamu iliyotua kichwani mwa Mbwana Samatta na kuandika bao la kuongoza.

Baada ya bao hilo Kocha Mayanga alifanya mabadiliko katika eneo la kiungo kwa kumtoa Himid Mao Mkami na kumuingiza Mudathir Yahya Abbas.
DR Congo walijisahau wakidhani kwamba wanaweza kurudisha bao hilo, Stars walifanikiwa kupata bao la Pili katika dakika ya 86 kwa shuti kali nje ya 18 kupitia kwa Shiza Kichuya baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa nahodha Mbwana Samatta.

Baada ya bao hilo Kichuya alikwenda benchi na nafasi yake ikachukuliwa na mchezaji wa kimataifa Rashid Mandawa, pia Simon Msuva akatoka na kuingia Yahaya Zayd.

Mpaka mchezo huo unamalizika Tanzania walitoka kifua mbele kwa ushindi mnono wa mabao 2-0 dhidi ya timu ngumu ya DR Congo.

Mchezo huo ni wa pili wa kirafiki katika kalenda ya Shirikisho la Soka Ulimwengu FIFA, baada ya ule wa awali kufungwa kwa mabao 4-1 dhidi ya timu ya Taifa ya Algeria.

Tanzania : Aishi Manula, Shomari Kapombe, Gadiel Michael Mbaga, Erasto Nyoni. Abdi Banda, Kelvin Yondani, Himid Mao, Mohamed Issa, Mbwana Samatta, Saimon Msuva na Shiza Kichuya.
Akiba : Ramadhan Kabwili, Mohamed Abdulrahman, Hassan Kessy, Erasto Nyoni, Mudathir Yahya, Said Ndemla, Ibrahim Ajib, Feisal Salum, Yahya Zayd, Shaban Idd Chilunda na Rashind Mandawa.

DR Congo: Ley Matampi, Issam Mpeko, Glody Ngoda, Yannick Bangala, Wilfred Moke, Aaron Tshibola/Lema Mabidi, Chancel Mbemba, Mubele Ndombe, Needkens Kebano, Benick Afobe, Yannick Bolasie.
Akiba: Antony Mossi, Nathan Mabroul, Lema Mabidi, Junior Kabananga, Assombalanga Britt, Chadrac Akolo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox