STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 8 Aprili 2015

CHELSEA YAIZODOA ARSENAL KUHUSU CECH.

KLABU ya Chelsea imeitaarifu Arsenal kuwa hawatarajii kuwauzia golikipa wao Petr Cech katika kipindi cha majira ya kiangazi. Arsenal imekuwa ikitafuta golikipa mpya na kumuangazia Cech ambaye anategemewa kuondoka majira ya kiangazi baada ya kupoteza namba katika kikosi cha kwanza cha Chelsea mbele ya Thibaut Courtois msimu huu. Hata hivyo, Chelsea hawataki kuwauzia Arsenal golikipa huyo kwa hofu ya kuwaimarisha mahasimu wao hao msimu ujao wa Ligi Kuu. Pamoja na taarifa hizo Arsenal itajaribu kutuma ofa ya euro milioni 14 kujaribu kumsajili golikipa huyo ingawa wanajua itakuwa ngumu kumpeleka Emirates. Chelsea wameshakubali kuwa Cech anataka kuondoka na kutafuta timu atakayopata nafasi ya kucheza lakini wako radhi kumuuza nje ya Uingereza huku Paris Saint-Germain ikiwa miongoni mwa vilabu vinavyotajwa kumtaka golikipa huyo mwenye umri wa miaka 32

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox