STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumapili, 5 Aprili 2015

MAN UNITED YAPEWA OFA YA KUMSAJILI KHEDIRA.

KLABU ya Manchester United imepewa ofa ya kumsajili kiungo wa Real Madrid Sami Khedira lakini kama watakubali kumlipa kitita cha paundi 200,000 kwa wiki. Kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani anatarajiwa kumaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu na United wamegutushwa juu ya suala hilo. Hata hivyo, United wao wamelenga zaidi kutaka kumsajili kiungo wa AS Roma Kevin Strootman ambaye hata hivyo bado majeruhi. Kama United ikifanikiwa kumsajili Khedira mwenye umri wa miaka 28, atakuwa mchezaji wa kwanza kutoka Ujerumani kuitumikia klabu hiyo. United wanaweza kukabiliwa na upinzani kutoka kwa Chelsea kwani Jose Mourinho ambaye amewahi kumfundisha Khedira akiwa Madrid naye amekuwa akimhusudu mchezaji huyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox