STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 3 Septemba 2015

KIPINDI CHA MAVUNO KWA JORGE MENDES.......




Ikiwa dirisha la usajili limefungwa barani Ulaya, kila klabu inajiandaa kupiga mahesabu ni kiasi gani cha fedha imetumia kwa ajili ya kufanya usajili. 

Lakini wakati vilabu vikipiga hesabu ya kiasi gani imetoa na kuingiza wakati wa usajili, kuna mtu anaitwa Jorge Mendes yeye wakati huu, huwa anapiga hesabu ya kiasi alichoingiza.

jorge-mendes_3023686b

Jorge akiwa na Radamel Falcao ni wakala wake pia

Jorge Mendes ni wakala maarufu ambaye anafanya shughuli hiyo kwa wachezaji kadhaa, huwa anatanguliza maslahi mbele kuliko kitu kingine chochote. Kati ya mwaka 2001 hadi 2010 amehusika kwa asilimia 68 katika kila usajili wa kuuza wachezaji kutoka vilabu vya Benfica,Porto na Sporting Lisbon za Ureno.

1356645085_extras_mosaico_noticia_1_g_0

Ni wakala wa Pepe pia

Mreno huyu kwa hivi siku za karibuni amekuwa ana husika kwa nafasi kubwa katika usajili unaofanywa na vilabu vya Atletico MadridDeportivo La CorunaMonaco na Valencia. Huyu ndiye wakala ambaye mara nyingi ufaidika katika uhamisho wa masaa kadhaa kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

1356645085_extras_mosaico_noticia_1_g_0

Haikuwa safari rahisi kwa Jorge Mendes kuwa wakala mkubwa wa wachezaji wa kubwa, safari ilianza mwaka 1996 kwa mteja wake wa kwanza Nuno walipo kutana katika Bar ya Guimaraes na kufanikisha uhamisho wa Nuno kwenda katika klabu ya Deportivo . Mendes ni wakala wa Cristiano Ronaldo na wachezaji wengine wengi.
Diego Costa ni moja kati ya wateja wa Mendes hiki ni kitu alichowahi kufanyiwa na Mendes katika masuala ya usajili.

Manchester-City-vs-Chelsea

“Jorge aliniambia natakiwa kupanda ndege na kwenda Madrid lakini nilikuwa sijui nini kinaendelea nilivyofika aliniambia alikuwa anasaini Atletico Madrid, baadae akaniambia kuwa tulikuwa katika nyumba ya mkurugenzi wa michezo wa Atletico Madrid  Jesús García Pitcarch nilikuwa simjui hata kidogo”>>> Diego Costa

*** Local Caption *** BEBE-AGENT: Jorge Mendes er agenten til blant annet Manchester Uniteds Nani.

Ameshawahi kusimamia uhamisho wa Luis Nani

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Jorge Mendes ndiye wakala aliyepewa zawadi ya kisiwa  na Cristiano Ronaldo katika harusi yake, kupitia biashara hiyo katika kipindi cha miaka 20, Mendes anatajwa kuingiza kiasi cha pound bilion 1 na anatajwa kama wakala ambaye mipango yake ya uhamisho mingi huwa inafanikiwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox