STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 12 Novemba 2015

BLATTER HOI HOSPITAL.

RAIS wa Shirikisho la Soka la Duniani-FIFA, Sepp Blatter amelazwa hospitalini kutokana na kupatwa mshituko wa neva. 
 
Blatter aliyesimamishwa kwa siku 90 kujishughulisha na masuala ya soka wakati akichunguzwa kwa kashfa za rushwa , alilazwa hospitalini kwa ajili ya uchunguzi wa afya lakini sasa imeelezwa ataendelea kubaki huko. 
 
Blatter aliyeongoza shirikisho hilo kwa miaka 18 mpaka sasa, awali ilidaiwa alikuwa na matatizo ya msongo wa mawazo hivyo ikabidi apate huduma ya matabibu, sasa imebainika ana tatizo la mshituko wa neva. 
 
Awali, mwanasheria wake, Richard Cullen alieleza juu ya uangalizi huo wa madaktari kutarajiwa, lakini akasema alitarajia arejee nyumbani mapema kabla hali kubadilika na kutolewa maelezo tofauti. 
 
Hata hivyo, watu wake wa karibu wameeleza hali yake si mbaya na anatarajiwa kurejea katika hali ya kawaida japokuwa atabaki hospitalini hadi mapema wiki ijayo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox