STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 12 Novemba 2015

FIFA WAANZA KUCHUJA MAJINA YA WAGOMBEA URAIS, MUAFRIKA AKATWA, WAMEBAKI WATANO

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limelichuja jina la rais wa Shirikisho la Soka la Liberia, Musa Bility katika kinyang’anyiro cha urais wa shirikishi hilo. 
 
FIFA limepitisha majina ya wagombea watano wa nafasi hiyo huku jina la rais wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA Michel Platini aliyesimamishwa likiwa halijajumuishwa. 
 
Platini raia wa Ufaransa jina lake linaweza kuongezwa katika orodha hiyo kama adhabu yake ya kusimamishwa itakwisha kabla ya Februari ambapo uchaguzi utafanyika. 
 
Majina matano yaliyopitishwa ni pamoja na Prince Ali bin al-Hussein, Jerome Champagne, Gianni Infantino, Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa na Tokyo Sexwale. 
 
Katika maelezo yake FIFA haikufafanua kwanini haswa walimkata Bility lakini anaweza kukata rufani kupinga uamuzi huo katika Mahakama ya Kimataifa ya Michezo-CAS.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox