Mchezaji mpya, Diego Costa akijiandaa kupokea mpira wakati wa mazoezi ya Chelsea kujiandaa na msimu nchini Austria
Cesc Fabregas (katikati) akifanya mazoezi na Chelsea
WACHEZAJI
wapya Diego Costa na Cesc Fabregas wameanza kujifua na timu yao mpya,
Chelsea inayofundishwa na Mreno Jose Mourinho ambayo imepiga kambi
Austria.
Wawili
hao walioajiliwa kutoka Atletico Madrid na Barcelona msimu huu,
walionekana wenye furaha na moral ya hali ya juu wakati wa mazoezi yao
ya kwanza baada ya kufanya vibaya Kombe la Dunia wakiwa na timu yao
ya taifa, Hispania.
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho (wa pili kulia) akiongoza mazoezi
Wabrazil, Diego Costa na Filipe Luis walipowasili Chelsea
Kikosi cha Chelsea kilichopo kwenye kambi hiyo kinaundwa na Petr Cech, Matej Delac, Mitchell Beeney, Mark Schwarzer, Branislav Ivanovic, Oriol Romeu, Kurt Zouma, Andreas Christensen, John Terry, Gary Cahill, Nathan Ake, Cesar Azpilicueta na Marco van Ginkel. Wengine ni Nemanja Matic, Nathaniel Chalobah, Mohamed Salah, Jeremie Boga, Lewis Baker, John Swift, Cesc Fabregas, Patrick Bamford, Fernando Torres, Diego Costa, Dominic Solanke, Filipe Luis na Isaiah Brown.
ZIARA YA CHELSEA KUJIANDAA NA MSIMU
Julai 23, 2014: Wolfsberger AC
Julai 27, 2014: Olimpija
Julai 30, 2014: Vitesse
Agosti 3, 2014: Werder Bremen
Agosti 10, 2014: Ferencvaros
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni