Viungo mbali mbali vya binadamu vimekutwa katika eneo
la kutupa taka la Bunju mjini Dar es Salaam katika mazingira ambayo
haijafahamika mara moja kuwa viungo hivyo vimetoka wapi.
Kwa mjibu wa Afisa mmoja wa polisi ambaye
hakutaka jina lake litajwe amesema viungo hivyo vya binadamu
vilivyokutwa ni miguu,vidole ambavyo vilikutwa vikiwa vimefungwa ndani
ya mifuko.
Hata pamoja na viungo hivyo pia vifaa vya upasuaji vimekutwa zikiwemo glovuzi.
Mtu mmoja anashikiliwa kuhusishwa na tukio hilo
ambaye ni dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo lililobeba viungo hivyo
vya binadamu.
Haijafahamika mara moja miili hiyo
ya binadamu imetolewa wapi na ilipelekwa eneo hilo kwa lengo gani.
Katika miaka ya hivi karibuni Tanzania imekuwa
ikikabiliwa na tatizo la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi albino
ambapo viungo vyao huchukuliwa,japo kuwa viungo hivi vilivyokutwa kwa
sasa bado havihusishwi moja kwa moja na matukio ya mashambulizi na
mauaji ya walemavu hao.
Kwa mujibu wa Radio One:
Jeshi la Polisi wilaya ya Kinondoni limesema kuwa limekamata viungo mbalimbali vya binadamu vilivyohifadhiwa ktk mifuko ya plastiki ktk machimbo ya kokoto ya Bunju nje kidogo ya jiji la Dsm
Taarifa za tukio hilo zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura.
Uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea na taarifa zaidi kuhusu tukio hili zitaendelea kuwajia.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni