Manchester United imetoa Ofa ya mwisho kwa Juventus ya Pauni Milioni
39 kumnunua Kiungo wao, Juventus, kwa mujibu wa Jarida la Michezo la
Italy, Tuttosport.
Ofa hiyo, ya staili ya: 'Chukua Hutaki Basi', inaaminika inaweza kufungua milango kwa Juventus kukubali kumuuza Kiungo wao mahiri kutoka Chile alieng’ara sana huko Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
Vidal alijiunga na Juve Mwaka 2011 na kila Mwaka ameisaidia sana Klsbu hiyo kuibuka Mabingwa wa Italy.
Hadi sasa Juve wamekuwa wagumu kumuachia Vidal lakini ofa hii pamoja na imani kwamba Mchezahi huyo anataka kuondoka vinaweza kuwanufaisha Man United.
Hivi sasa Vaidal amebakisha Miaka Mitatu kwenye Mkataba wake na Juve.
Wiki iliyopita Gazeti moja huko Nchini kwao Chile liliripoti kuwa Mchezaji huyo anawindwa na Man United.
Akiongea na Gazeti la El Mercurio Vidal alisema: “Nimesikia uvumi huu lakini sitaki kuongelea. Kwa sasa nipo vakesheni na nikirudi Italy tutaona.”
Aliongeza: “Manchester United? Nimepoa lakini ukweli nani hatapendezewa ikiwa moja ya Klabu kubwa Duniani inamtaka?”
Vidal aliichezea Nchi yake Chile huko Brazil na wakatolewa Raundi ya Pili na
Brazil kwa Mikwaju ya Penati.
Kabla ya kutua Juve, Vidal alikuwa huko Germany akiichezea Bayer Leverkusen na kuhamia Juve Mwaka 2011 na kutwaa Ubingwa wa Italy mara 3.
Tayari Man United, chini ya Meneja wao mpya Louis van Gaal, imeshanunua Wachezaji wawili wapya, Fulbeki Luke Shaw na Kiungo Ander Herrera.
Wakati huo huo, Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa Man United, Ed Woodward, amesisitiza kuwa wao wako tayari kuvunja Rekodi ya kununua Mchezaji kwa bei yeyote ile ikiwa tu Mchezaji huyo atatakiwa na Meneja Van Gaal.
Woodward amesema uwezo wa kifedha upo na Klabu haiogopi kutumia kiasi chochote cha Fedha kununua Wachezaji watakaowafaa.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni