Katibu wa Yanga SC, Benno Njovu kushoto akibadilishana Mikataba na Jaja leo baada ya kusaini |
MSHAMBULIAJI Geilson Santos Santana ‘Jaja’ kutoka Brazil leo amesaini mkataba wa miaka miwili (2014-2016) kuitumikia klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam.
Katibu mkuu wa Yanga SC, Beno Njovu amesema usajili wa Jaja unakuwa ni wa pili msimu huu kwa wachezaji wa kigeni, baada ya awali kumsajili kiungo mshambuliaji Andrey Coutinho ambaye pia ni raia wa Brazil.
"Kazi
yetu uongozi ni kutekeleza maelekezo ya kocha mkuu pamoja na benchi la
ufundi, walitoa mapendekezo ya usajili kabla hawajaanza kazi na mengine
baada kuwasili yote tunajitahidi kuyatekeleza ili kila kitu kiende safi"
alisema Beno.
Jaja, ambaye alizaliwa tarehe 21 Septemba 1985 na kukulia katika mji wa Aracaju nchini Brazili mpaka anasajiliwa na timu ya Yanga alikuwa akiichezea timu ya Itabaina FC iliyopo nchini Brazil.
Yanga sasa inatakiwa kuacha mchezaji mmoja wa kigeni kati ya wanne waliobaki kutoka kikosi cha msimu uliopita ambao ni Wanyarwanda beki Mbuyu Twite na kiungo Haruna Niyonzima na Waganda washambuliaji Emanuel Okwi na Hamisi Kiiza.
Kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara zinaagiza wachezaji wa kigeni wawe watano na kwa Yanga kuzidisha idadi watalazimika kumpunguza mmoja.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni