STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 12 Julai 2014

KOMBE LA DUNIA: WAGOMBEA ‘MPIRA WA DHAHABU’, ‘GLOVU YA DHAHABU’ WATAJWA!

FIFA imetangaza Majina ya Wagombea Tuzo za aina 3 za Mchezaji Bora wa Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil.

‘MPIRA WA DHAHABU’
NEYMAR-BRAZIL-CAMEROONFIFA imetangaza Majina ya Wachezaji watakaogombea Tuzo ya Mchezaji Bora wa Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil, Tuzo ya Mpira wa Dhahabu.MESSI_IN_ARGENTINA
Listi hiyo ya Wachezaji 10 inao Wachezaji Wanne kutoka Germany, Watatu wa Argentina huku Colombia, Brazil na Netherlands zikitoa Mchezaji mmpja moja.
Wachezaji wa Argentina ambao wako kwenye Lisi hiyo ni Angel Di Maria, Javier Mascherano na Lionel Messi.
Germany ni Mats Hummels, Toni Kroos, Phillip Lahm na Thomas Muller.
Waliobaki ni Straika wa Colombia James Rodriguez, Staa wa Brazil Neymar na Arjen Robben wa Netherlands.
‘GLOVU YA DHAHABU’
Vile vile FIFA imateja Majina ya Makipa Watatu ambao watawania Tuzo ya Kipa Bora wa Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil.
Kipa Bora atapewa Tuzo ya Glovu ya Dhahabu.
Makipa hao ni Kipa wa
Costa Rica Keylor Navas, Manuel Neuer wa Germany na Kipa wa Argentina Sergio Romero.
‘MCHEZAJI BORA KIJANA’
Pia, Straika wa Netherlands Memphis Depay pamoja na Paul Pogba na Raphael Varane wa France wameteuliwa kugombea Tuzo ya Mchezaji Bora Kijana.
WASHINDI
Washindi wote wa Tuzo hizo watatangazwa mara baada ya Fainali ya Jumapili kati ya Argentina na Germany huko Estadio Maracana, Rio de Janeiro.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox