Bao tamu: Robert Lewandowski akipitisha mpira juu ya mabeki na kipa wao kufunga bao zuri
MCHEZAJI
mpya wa Bayern Munich, Robert Lewandowski jana ameendelea kung'ara
katika timu yake mpya baada ya kufunga bao zuri katika safe ya 2-2 na
Borussia Monchengladbach mchezo wa kujiandaa na msimu.
Mshambuliaji
huyo wa Poland aliyetua kama mchezaji huru kutoka wapinzani wao wa
Bundesliga, Borussia Dortmund -tayari amefunga mabao mawili tangu
awasili.
Bao la pili ni la jana alipomtungua kipa mbele ya mabeki wake wanne ndani ya boksi.
Siku za furaha: Lewandowski akipongezwa na mwenzake Franck Ribery aliyerejea Bayern baada ya kupona
Na
baada ya Bayern kutoa safe ya 2-2 mchezo ulihamia kwenye mikwaju ya
penalti, ambako walishinda, na ilikuwa ni furaha mno kwa Franck Ribery
aliyerejea uwanjani baada ya kupona maumivu yaliyomfanya akose fainali
za Kombe la Dunia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni