Raha tupu: Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney akimpongeza Danny Welbeck baada ya kufunga bao la kwanza.
LOUIS Van Gaal ni kiboko. Awaonya Jose Mourinho na Asernal Wenger kuwa amekuja kufanya kazi Old Trafford.
Jana usiku ameshusha majanga kwa LA
Galaxy baada ya kuitandika mabao 7-0 katika mchezo wa kirafiki wa
maandalizi ya kabla ya Msimu nchini Marekani.
Hii imezidi sasa! Van Gaal atakuwa
anawaomba viongozi wa Manchester United kuipeleka timu kwenye ziara ya
maandalizi ya kabla ya msimu kila majira ya kiangazi.
Ikiwa ni siku moja tu imepita tangu
alalamike kuhusu ziara ya Marekani kwa madai kuwa inawafanya wachezaji
wake wachoke, kocha huyo mpya wa Man United aliitazama timu yake ikipata
ushindi mkubwa na kuonesha kiwango kizuri.
Mabao ya Man United yalifungwa na
Welbeck dakika ya 13, Rooney dakika ya 41 (kwa penati) na dakika ya 45.
Mengine yalifungwa na James dakika ya 62, 84 na mawili ya mwisho
yalifungwa na Young katika dakika za 88 na 90.
Kikosi cha Man United kipindi cha kwanza (3-4-3): De Gea; Smalling, Jones, Evans; Valencia, Fletcher, Herrera, Shaw; Mata; Welbeck, Rooney.
Kikosi cha Man United kipindi cha pili (3-4-3): Lindegaard; M Keane, Fletcher, Blackett; Rafael, Cleverley, Herrera, James; Kagawa; Nani, Young.
Kiosi cha LA Galaxy: Penedo; Gargan, Meyer, Leonardo, DeLaGarza; Ishizaki, Sarvas, Juninho, Husidic; Keane, Zardes.
Alioneshwa kadi ya njano: Keane, Leonardo.
Mwanzo mzuri: Welbeck akishangilia baada ya kuifungia Man United goli la kuongoza katika dakika ya 13
Rooney akimfunga kipa Jaime Penedo kwa mkwaju wa penati na kuandikia bao la pili kwa Man United.
Van Gaal akitazama mechi akiwa kwenye benchi na msaidizi wake Ryan Giggs
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni