KOCHA
Jose Mourinho amesema Chelsea imemaliza usajili wa kununua wachezaji na
sasa anataka kupandisha chipukizi kutoka timu za vijana.
The
Blues imemwaga fedha kuwasajili Cesc Fabregas, Diego Costa na Filipe
Luis, na kwa muda mrefu haijapndisha mchezaji kutoka kwenye
akademi yake tangu Nahodha wake wa muda mrefu, John Terry.
Lakini
kocha Mourinho amesema kwamba wachezaji hao wapya wanatosha kuongeza
nguvu katika kikosi kilichofika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu
uliopita.
CHIPUKIZI WATANO WA KUMULIKWA CHELSEA
1. Jeremie Boga
2. Izzy Brown
3. Patrick Bamford
4. Marco Van Ginkel
5. Kurt Zouma
Alipoulizwa kama kikosi chake kitakuwa na sura mpya zaidi Stamford Bridge, Mourinho alisema: "Sifikirii hivyo".
"Soko lipo wazi, lakini tuna furaha na tulichonacho. Tunafikiri kwamba, kikosi chetu ndicho tulichokitaka.
"Hatutaki
kikosi cha wakongwe watupu, pia tunataka kuingiza katika kikosi cha
kwanza wachezaji watatu, wanne au watano wa U-21na kuendeleza wachezaji,
hivyo tuna furaha na uwiano uliopo ndani ya kikosi,".
Chipukizi
wa Chelsea wamekuwa kivutio katika mechi za kujiandaa na msimu, Jeremie
Boga akiinusuru The Blues kulala katika mchezo wa kwanza wa ziara ya
kujiandaa na msimu nchini Austria dhidi ya RZ Pellets akifunga bao
lililofanya sare, wakati Patrick Bamford na Izzy Brown wote walifunga
dhidi ya Wycombe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni