Amesaini: Didier Drogba amesaini mkataba wa mwaka mmoja Chelsea
Mshambuliaji huyu wa Ivory Coast amekamilisha vipimo vya afya na kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Chelsea.
Didier Drogba amekamilisha ndoto za kurejea Chelsea.
Nyota huyo wa Ivory Coast amesaini mkataba wa mwaka mmoja Stamford Bridge.
Gwiji huyu alisainiwa kwa mara ya kwanza klabuni hapo na Jose Mourinho kwa dau la paundi milioni 24 mwaka 2004.
Drogba amefichua siri kuwa hakutaka kupoteza nafasi ya kufanya kazi tena na kocha Mourinho kwa mara nyingine tena.
Alisema: "Yalikuwa maamuzi
rahisi-nisingeweza kupoteza nafasi ya kufanya kazi tena na Jose. Kila
mtu anajua mahusiano mazuri niliyokuwa nayo na klabu hii, na mara zote
nimekuwa nikijisikia kama nyumbani".
Amerudi: Didier Drogba amerudi London Magharibi baada ya kucheza China na Uturuki.
"Hamu yangu bado ni ileile na naangalia
mbele kuisaidia timu hii. Namefurahia sana ukurasa huu mwingine wa
maisha yangu ya soka".
Mourinho amewaondoa hofu mashabiki wa
klabu hiyo akisisitiza kuwa Muivorycost huyo bado ni mshambuliaji bora
katika ulimwengu wa soka.
"Amekuja kwasababu ni miongoni mwa
washambuliaji bora Ulaya. Namjua sana na najua kuja kwake hajivunia
historia yake au kile alichofanya klabuni miaka ya nyuma", Alisema
Mourinho.
Mchezo wa mwisho kwa Drogba akiwa
Chelsea ulikuwa wa UEFA ambao alifunga penati ya ushindi na kutwaa kombe
hilo dhidi ya Bayern mwaka 2012.
Drogba amerudi Chelsea baada ya kucheza miaka miwili nje ya London
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni