STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumapili, 20 Julai 2014

RAIS WA URUGUAY: ‘SUAREZ ANAHITAJI DAKTARI WA MAGONJWA YA AKILI SI KIFUNGO!’

RAIS wa Uruguay, Jose Mujica, ameponda Kifungo cha Mchezaji wa Nchi hiyo Luis Suarez cha Miezi Minne alichopewa na FIFA na badala yake anahitaji msaada wa Madaktari wa Magonjwa ya Akili.
RAIS-MUJICA-URUGUAYSuarez alifungiwa Miezi Minne kutojishughulisha na chochote kuhusu Soka na pia kufungiwa Mechi 9 za Uruguay baada kupatikana na hatia ya kumuuma Meno Beki wa Italy, Giorgio Chiellini, wakati wa Mechi ya Kombe la Dunia kati ya Uruguay na Italy huko Brazil hapo Juni 24.LUIS_SUAREZ-KILIO
Akiongea na Gazeti la Brazil, Folha de Sao Paulo, Rais Mujica, ambae ndie anasifika ya kuwa Rais ‘maskini’ kupita yeyote Duniani kwa uamuzi wake wa kuishi kwenye Banda la Shambani kwake badala ya Ikulu akilindwa na Polisi Wawili tu na Mbwa wake Manuela mwenye Miguu Mitatu, amesema: “Anatoka Familia fukara na akili yake ni Miguu yake. Ni bora kumpeleka Hospitali ambako atapata msaada wa Daktari wa Magonjwa ya Akili!”
Rais Mujica amefafanua: “Ni wehu kumfungia Mtu
asishiriki lolote kuhusu Soka! Hata Serikali haina mamlaka ya kumzuia Mtu asiingie Uwanja wa Mpira bila kupata Saini ya Jaji! Lakini FIFA wanakuja wanamfungia Miezi Minne bila hata kuwa na Jopo la Kisheria!”
Hivi sasa Suarez ameihama Klabu yake Liverpool ya England na kutua Barcelona ya Spain.
Na Rais Mujica amenung’unika: “Sasa tutamuona Suarez akicheza pamoja na Neymar na Messi lakini sijui lini itakuwa hivyo!”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox