KLABU
ya Chelsea ipo kwenye nafasi nzuri ya kumsaini Sami Khedira baada ya
jana usiku wakala wake kusema hakuna makubaliano yaliyofikiwa na
Arsenal
.
.
Kocha
wa Blues, Jose Mourinho amemsajili beki wa kushoto Filipe Luis kutoka
Atletico Madrid kwa Pauni Milioni 18 na kuhamishia nguvu zake kwa kiungo
wa Ujerumani, Khedira.
Ilikuwa
inafahamika Arsenal ilikubali kutoa Pauni Milioni 20 kwa Real Madrid
kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, lakini walikuwa
wanasuasua kufika kiwango cha mshahara anaotaka, Pauni 180,000 kwa wiki.
Pamoja
na hayo, wakala wa Khedira, Jorg Neubauer amesema: "Hatupo katika
mazungumzo na Arsenal. Sifikiri wanweza kukubaliana ada, vinginevyo
ningeambiwa,".
Khedira anavutiwa na Mourinho tangu anafundisha Real na kocha huyo inafahamika pia anampenda sana mchezaji huyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni