STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 6 Agosti 2014

JONAS MKUDE NJE WIKI SITA SIMBA SC

Jonas Mkude kushoto akiwa mchezaji mwenzake wa Simba SC, Ramadhani Singano 'Messi'

KIUNGO wa Simba SC, Jonas Mkude atakosa mechi kadhaa za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti.
Mkude aliumia akiichezea timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars mwezi uliopita nchini Botswana na baada ya vipimo mjini Dar es Salaam ikagundulika maumivu yake ni makubwa.
Baada ya kupatiwa matibabu, Mkude amesema; “Nimeambiwa natakiwa nipumzike wiki sita, na sasa nipo katika wiki ya pili,”alisema Mkude akizungumza na BIN ZUBEIRY jana Dar es Salaam.
“Kwa kweli nahitaji kutulia nipone kabisa ili nirudi uwanjani nikiwa fiti kabisa, sitaki kuharakisha ili niwe na matatizo ya kudumu. Nataka nipone vizuri kabisa ndipo nirudi uwanjani kwa nguvu mpya,”ameongeza.
Mkude ataanza mazoezi mepesi mwishoni mwa Septemba mwaka huu kipindi ambachio Ligi Kuu itakuwa inaanza (Septemba 20)- maana yake atatarajiwa kuanza kucheza taratibu mwezi mmoja baadaye
Kuumia kwa Mkude si pigo kwa klabu yake Simba SC, bali hata Taifa Stars ambayo kwa wakati huu inamkosa pia kiungo mwingine, Frank Domayo ambaye pia ni majeruhi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox