
RASMI wanachama wa klabu ya Simba sc wapatao 680
wamelazimika kuwafuta uanachama wanachama wenzao 72 waliokwenda mahakamani akiwemo
mgombea aliyeenguliwa katika uchaguzi uliopita, ‘Kidume’ Michael Richard
Wambura.
Maamuzi hayo yemefikiwa katika mkutano mkuu wa
kawaida wa klabu ya Simba uliofanyika leo katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa
Polisi, Osterbay jijini Dar es salaam.
Mbali na wanachama kujadili masuala muhimu na
kupokea taarifa mbalimbali za klabu katika mkutano huo, Agenda ya wanachama 72
waliokwenda mahakamani ndio ilibebea uzito wa juu zaidi na kila mtu alikuwa na
hamu ya kutaka kujua nini hatima ya Wambura na wenzake.
Wambura aliipeleka Simba mahakamani mwaka 2010 na
suala hilo lilisababisha kuenguliwa kwa jina lake katika uchaguzi mkuu wa Simba
na kamati ya uchaguzi chini ya mwenyekiti wake, Wakili Dkt. Damas Daniel
Ndumbaro.

Makamu wa Rais wa Simba sc, Geofrey Nyange 'Kaburu'
Lakini alikata rufani katika kamati ya Rufani ya
shirikisho la soka Tanzania TFF, chini ya mwenyekiti wake, Jaji Julius Mutabazi
Lugaziya na kushinda, hivyo kurejeshwa kwenye mchakato.
Sababu kubwa kumrudisha ilikuwa ni kwamba, tangu
Simba itangaze kumsimamisha uanachama Wambura mwaka 2010, ilimuacha huru na
kuendelea kushiriki shughuli za klabu kama mwanachama hai ikiwemo kulipia ada
ya kadi yake ya uanachama.
Lakini kamati ya Ndumbaro ilimuengua tena
kwasababu ya kupiga kampeni kabla ya muda.
Kutokana na nguvu kubwa aliyonayo Wambura,watu
walisubiri kujua nini itakuwa hatima yake leo hii.
Mtandao huu umezungumza na makamu wa Rais wa
Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ambaye amethibitisha kufutwa uanachama wanachama
72 pamoja na Wambura.
“Kikao kilikuwa kizuri na kimeendeshwa na Rais
wetu Bwana Evans Aveva. Wanachama wamepata nafasi ya kujadili masuala ya msingi
na wamepokea taarifa mbalimbali, lakini vilevile kuna maamuzi ambayo
yalifanyika,” alisema Kaburu.

Michael Richard Wambura amefukuzwa uanachama TFF
“Kulikuwa na agenda kubwa ambayo ilibeba uzito
mkubwa sana katika kikao cha leo ni ile ya wanachama 71 waliokwenda mahakamani.
“Ikimbukwe kuwa mwaka 2010, Bwana Michael Richard
Wambura na Bwana Nchemi walikwenda mahakamani na hadi sasa walikuwa hawajawi
kuzungumza kwenye mkutano mkuu.”
“Vilevile katika mkutano mkuu wa 2014, kuna
wanachama 70 waliokwenda mahakamani kuhusu masuala ya uchaguzi, kwahiyo leo kwa
kauli moja wanachama wa klabu ya Simba wapatao 680 waliohudhuria kikao wamelaizimika
kuwafuta wanachama hao waliokwenda mahakamani”
“Kitendo walichofanya ni utovu wa nidhamu, kwa
mujibu wa katiba ya klabu yetu ya Simba, ibara ya 55 inasema mwanachama anayekwenda
mahakamani basi afutwe uanachama wake”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni