Mshambuliaji nyota wa Man
City, Sergio Aguero amemuambia rafiki yake atakuwa nje kwa mwezi mzima kutokana
na maumivu ya goti.
Aguero aliumia katika mechi
ya Ligi Kuu England dhidi ya Everton.
Tayari Man City
imeshatangaza kuwa ameondolewa kwenye kikosi kitakachopiga katika mechi ya Ligi
ya Mabingwa Ulaya dhidi ya AS Roma, Jumatano.
Hata hivyo, imeelezwa Aguero atafanyiwa vipimo ndani ya siku chache ambavyo vitaamua matibabu yake yafanyike kwa muda gani na akae nje kwa kipindi kipi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni