|
Messi akishangilia moja ya mabao yake leo |
|
Suarez na Pique wakishangilia bao la pili la Barcelona |
|
Kabakisha hat trick mbili tu kumkuta Ronaldo |
|
Akipongezwa na Neymar |
|
Bravo Brother! |
|
Utukuzwe uliyenijalia kipaji hiki cha soka |
STRIKA Lionel Messi amejibu hat trick ya Cristiano Ronaldo baada ya
kufunga magoli matatu wakati akiisaidia Barcelona wakiiangamiza
wapinzani wa Jimbo la Cataluna, Espaniol kwa mabao 5-1 katika mechi ya
La Liga usiku huu.
Messi amefunga mabao hayo na kufanya afikishe jumla ya mabao 256 na
kuzidi kumuacha mbali Ronaldo aliyefikisha mabao 200 jana usiku.
Wageni Espanol walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa dakika ya 13
na Sergio GarcÃa kabla ya Messi kusawazisha kabla ya mapumziko.
Mkali huyo alifunga bao la pili dakika ya 50 akimalizia kazi ya Suarez
kabla ya Gerrard Pique kuongeza bao la tatu dakika ya 53 kwa kichwa na
Pedro kuongeza la nne dakika ya 77.
Messi alifikisha hat trick ya 21 na hat trick ya tatu katika mechi nne
tofauti zilizopita katika dakika ya 81 kwa kazi nzuri ya Pedro na
kuifanya Barcelona kufikisha jumla ya pointi 34 na kukwea hadi nafasi ya
pili wakiiengua watetezi Atletico Madrid wenye 32.
katika mchezo mwingine mapema, SEvilla ikiwa ugenini ilinyukwa bao 1-0 na Rayo Vallecano
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni