Goran (kulia) akiwasili Uwanja wa Ndege wa JK Nyerere
KOCHA mpya wa Simba sc, Mserbia Goran Kapunovic
amewasili asubuhi ya leo majira ya saa 1:00 katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
Goran ametua kwa ndege ya Shirika la Qatar Airways
na baada ya kuwasili amesema amekuja kufanya kazi na sivinginevyo.
Hata hivyo kocha huyo anayerithi mikoba ya Patrick
Phiri amesema atazungumza mengi baada ya kumalizana na viongozi na kuanza kazi
yake.
Goran anatarajia kuiongoza Simba kwa mara ya kwanza katika mechi za kombe la Mapinduzi linaloanza kutimua vumbi kesho januari mosi mwakani
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni