![]() |
MESSI AKIZUNGUMZA NA RONALDO KATIKA HAFLA YA TUZO ZA BALLOND'OR... |
Cristiano Ronaldo ameweka
wazi kwamba mwanaye Ronaldo Jr ana ushabiki mkubwa kwa Lionel Messi.
Ronaldo amesema mara kadhaa
mwanaye huyo wa kiume amekuwa akifuatilia kuhusiana na Messi.
“Amekuwa akiangalia video
kadhaa za mabao ya Messi, anamuunga mkono,” alisema Ronaldo na kucheka.
Katika hafla ya tuzo za
Ballond’Or, Ronaldo Jr alipata nafasi ya kumsalimia Messi.
Baba yake alifanikiwa kushinda tuzo ya tatu ya dunia ikiwa anashinda kwa mara ya pili mfululizo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni