
Alexis Sanchez ndiye bora kwa mujibu wa bosi wa Man City
Manuel Pellegrini ameweka wazi mchezaji
ambaye anaamini ni bora zaidi nchini England...na cha kushangaza
hajamtaja mshambuliaji wa Manchester City,Sergio Aguero.
Kiukweli, bosi huyo wa City aliweka wazi
kuwa mchezaji bora wa EPL ni mkali wa Arsenal, Alexis Sanchez ambaye
alifunga na kutoa pasi ya mwisho katika ushindi wa Gunners wa 3-0 dhidi
ya Stoke City jumapili iliyopita.
Akizungumza na AS, Mchile huyo mwenye
miaka 61 alifafanua sababu inayomfanya aamini kuwa nyota huyo ndiye bora
kuwa ni kufunga magoli 12 na kutoa pasi za mwisho 7 tangu asajiliwe kwa
paundi milioni 32 kutoka Barcelona majira ya kiangazi mwaka jana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni