JOSE
Mourinho alijifunza mengi mjini Paris. Sio jana usiku, lakini ni mwaka
mmoja uliopita. Kumbuka alikutana tena na PSG katika mechi ya ligi ya
mabingwa na wakati huo Mreno huyo alikuwa anaijenga Chelsea.
David Luiz alifanya kosa lililowarudisha mchezoni PSG baada ya kusababisha goli, huku kipa Petr Cech akikosa la kufanya.
Mourinho
alisahihisha kosa hilo kwa kumuuza nyota huyo kwenda PSG kwa ada ya
uhamisho wa paundi milioni 50 na kuwa beki ghali zaidi duniani.
Jana Mbrazil huyo amefanya makosa tena na kuipa faida timu yake ya zamani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni