Mario Balotelli
haishi vituko, ameisaidia Liverpool kuibuka na ushindi bao 1-0 dhidi ya Besiktas
ua Uturuki katika mechi ya Ligi ya Europa.
Balotelli amefunga
lakini bado ni shidaa, maana alimpokonya mshambuliaji mwenzake Danny Sturridge
mpira.
Wakati ilionekana
mwamuzi Henderson
alitaka kumpa Sturridge lakii Balotelli akaonekana kutowaamini wenzake.
Ilikuwa ni dakika ya
85, alitaka uhakika. Hakujali kama Sturridge au wengine watachukia, akachukua
na kupiga na kweli akafunga.
Wakati Balotelli
anashangilia na wengine, wengine walikuwa wanafanya kazi ya kumpoza Sturridge
ambaye alikuwa na jazba.
Nahodha
hasa wa Liverpool, Steven Gerrard alikuwa akifanya uchambuzi kwenye
runinga na ITV. Kuhusu hilo, alimpongeza Balotelli kwa kufunga lakini
akasisitiza, haikuwa sahihi kugombea mpira kwa kuwa ilionyesha ni utovu
wa nidhamu.
Liverpool: Mignolet, Can, Skrtel, Sakho, Ibe, Henderson, Allen (Lovren 63), Moreno, Lallana (Sterling 77), Sturridge, Coutinho (Balotelli 63)
Subs not used: Ward, Lambert, Manquillo, Borini
Booked: Lovren
Goals: Balotelli 85' (pen)
Besiktas: Gonen, Kurtulus, Franco, Gulum, Ramon,
Hutchinson, Kavlak, Tore, Sosa (Ozyakup 60), Sahan (Frei 72), Ba
Subs not used: Fidayeo, Pektemek, Arslan, Uysal, Opare
Booked: Gulum, Kurtulus, Motta, Franco
Referee: Szymon Marciniak (Poland)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni