Klabu
ya Barcelona ya nchini Hispania leo imebadili jina la uwanja wake wa
mazoezi na kuupa jina la kocha wa zamani wa klabu hiyo Tito Vilanova
aliyefariki Aprili mwaka jana kwa ugonjwa wa kansa ya koo.Uwanja huo uliokuwa unafahamika kwa jina la Joan Gamper umepewa jina hilo ikiwa ni sehemu ya kumuenzi kocha huyo aliyeifundisha timu hiyo msimu wa 2012/2013.
Zoezi hilo la uzinduzi limefanyika leo asubuhi likuhudhiliwa na wachezaji na viongozi mbalimbali wa timu hiyo.
Pia
leo asubuhi kikosi cha kwanza cha Barcelona kimeutumia uwanja huo
kufanya mazoezi wakati wakijiandaa na mchezo wa La Liga hapo kesho dhidi
ya Malaga kwenye dimba la Camp Nou.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni