MSHAMBULIAJI nyota wa
kimataifa wa Ivory Coast, Wilfried Bony anaamini anaweza kuwa silaha ya
siri kwa Manchester City katika mbio zao za ubingwa wa Ligi Kuu wakati
akijiandaa kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Newcastle United
Jumamosi hii. Bony alijiunga na City inayonolewa na Manuel Pellegrini
akitokea Swansea City kwa kitita cha paundi milioni 28 Januari mwaka huu
lakini bado hajacheza mechi yeyote kutokana na majukumu ya kimataifa
aliyokuwa nayo katika michuano ya Mataifa ya Afrika. Sasa nyota huyo
mwenye umri wa miaka 26 atapata nafasi kwa mara ya kwanza kuwaonyesha
mashabiki wa City na kuwapa matumaini mapya ya kutetea taji lao. Bony
ambaye alifunga mabao 34 katika mechi 70 alizoichezea Swansea ana
uhakika kuwa anaweza kuisaidia timu hiyo kufikia malengo yake. City
wanashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi wakiwa nyuma ya vinara
ya Chelsea.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Ijumaa, 20 Februari 2015
BONY ATAMBA KUISAIDIA CITY KUTETEA TAJI LA LIGI KUU.
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni