MTANDAO mmoja barani
Ulaya umetoa taarifa kuwa tayari muafaka umeshafikiwa kwa michuano ya
Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Qatar mwaka 2022 kufanyika katika
kipindi cha Novemba na Desemba ili kuwepa joto kali katika kipindi cha
kiangazi. Wakiorodhesha vyanzo mbalimbali mtandao huo umedai kuwa uamuzi
umeshafanyika kwani kikosi kazi kilichoteuliwa na Shirikisho la Soka
Duniani-FIFA kinatarajia kuwasilisha miezi hiyo katika kikao chao
kitakachofanyika wiki ijayo jijini Doha kabla ya kamati ya utendaji
haijakamilisha mpango huo wakati wa kikao cha mwezi ujao jijini
Zurich. Wiki tatu zilizopita, katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke katika
mahoajiano yake na radio moja nchini Ufaransa alisema Kombe la Dunia
nchini Qatar linatakiwa kuandaliwa wakati wa majira ya baridi lakini
kugongana na michuano ya olimpiki ya kwenye baridi Februari mwaka 2022
pia ni hatihati. Hata hivyo mpango huo haujafafanua kwa undani zaidi
kuwa michuano ya Kombe la Shirikisho ambayo huchezwa mwaka mmoja kabla
ya Kombe la Dunia kama nayo itasogezwa mbele kuepuka majira ya
kiangazi. Desemba mwaka jana Chama cha Vilabu barani Ulaya na Muungano
wa Ligi za Soka barani humo vilipendekeza michuano hiyo ya Qatar
kuchezwa kati ya May na Juni ili kutovuruga ratiba zingine za kawaida za
msimu.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Ijumaa, 20 Februari 2015
KOMBE LA DUNIA MWAKA NCHINI QATAR KUFANYIKA NOVEMBA NA DESEMBA MWAKA 2022.
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni