Winga
wa klabu ya Liverpool Lazar Markovic sasa amefungiwa mechi nne baada ya
kuonyesha kitendo cha utovu wa nidhamu alipopewa kadi nyekundu katika
mchezo uliopita wa kombe la klabu Bingwa Barani Ulaya dhidi ya klabu ya
Fc Basel mwezi Disemba, ambapo mchezo huo ulimalizika kwa timu hizo
kutoa sare ya kufungana mabao moja kwa moja.
Markovic
mwenye umri wa miaka Ishirini, aliingia uwanjani akitokea benchi
kipindi cha pili katika mtanange huo, lakini alijikuta akizawadiwa kadi
nyekundu baada ya kumchezea rafu mbaya mchezaji Behrang Safari wa Fc
Basel.
Akizungumza
baada ya mchezo kocha wa klabu ya Liverpool Brendan Rodgers, alisema
akubaliani na maamuzi yaliyotolewa na Refa aliyekuwa anachezesha mchezo
huo, na kusema yalikuwa maamuzi mabovu na kusisitiza kuwa Markovic
akustahili kupewa kadi nyekundu.
"Kwa
kweli ni uamuzi ambao haukustaili kabisa kutolewa kwa mchezaji wetu
licha ya kufanya kosa kwani katika mchezo wa mpira wa miguu makosa kama
hayo huwa yanatokea na wachezaji wamekuwa hawapewi adhabu kama hii
ambayo inamdidimiza mchezaji kisoka," alisema Rodgers.
Kadi hiyo ya Markovic inamaanisha sasa mchezaji huyo ataikosa michezo inayofuata katika kombe la Uropa ambapo Liverpool ilishushwa kushiriki katika michuano hiyo baada ya sare waliyoipata.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni