Kiungo
mshambuliaji wa klabu ya borrusia Dortmund Marco Reus amesaini mkataba
mpya wa miaka mitatu utakaomuweka katika dimba la signal Iduna Park
mpaka mwaka 2019.
kiungo
huyo amekuwa akiwaniwa na klabu mbalimbali barani ulaya wakiwemo
mabingwa watetezi wa klabu bingwa barani ulaya Real madrid, Manchester
united, bayern munich pamoja na klabu ya manchester city, lakini sasa
Reus anatazamiwa kuendelea kukipiga na klabu hiyo chini ya kocha Jurgen
Klopp.
Reus mwenye umri wa miaka 25 alisema anafuraha sana kuendelea kucheza ligi kuu nchini ujerumani kwani ni ligi nzuri na yenye upenzani wa hali ya juu, licha ya kuonekana kama klabu ya bayern munich na borrusia dortmund ndizo zinazopeta katika ligi hiyo almaarufu kama bundasiliga.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni