STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 16 Februari 2015

MAYWEATHER ADAI KUWA NA HAMU KUZICHAPA NA PACQUIAO.

BINGWA wa masumbwi wa uzito wa welter anayeshikilia mikanda ya WBC na WBA, Floyd Mayweather amesema anatumaini pambano lake na Manny Pacquiao litawezekana lakini makubaliano bado hayajafikiwa. Mayweather mwenye umri wa miaka 37 raia wa Marekani na Pacquiao raia wa Filipino mwenye umri wa miaka 36, hivi karibuni walibadilishana namba katika moja ya michezo ya mpira wa kikapu nchini Marekani. Akiulizwa kuhusu tetesi za pambano lao, Mayweather amesema hakuna yeyote kati yao aliyesaini chochote kwani bado hawajafikia makubaliano. Mayweather aliendelea kudai kuwa kinachoendelea hivi sasa ni tetesi lakini ana matumaini pambano hilo linaweza kufanyika. Pambano la mabondia hao kama litafanikiwa linatajwa kuwa pambano bora kabisa katika kizazi cha sasa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox